06 February 2012

Freemasons-13

(Wanavyohusihwa na tukio la  9/11)



·Jumuiya inayotawala dunia kwa ‘mlango wa nyuma’

·Wanachama wake wengi ni wakuu wa nchi duniani




WIKI iliyopita tuliona kwamba, katika kudhihirisha kuwa Freemasons wanatawala ulimwengu hadi nemboo ya Umoja wa Mataifa (United Nations) imeundwa kwa alama na kielelezo cha Freemasons.

Katika elimu ya namba A = 1, B = 2, C = 3, D = 4, na kuendelea. Kuna sehemu 33 ndani ya nembo ya UN ambapo herufi U (21),  N (14) = (2+1=3) (1-4=3) 3 na 3 hivyo kufanya namba 33 ambalo ni daraja la juu kabisa katika Freemasons.

Kuna msemo wa maandiko unasomeka hivi "No one will enter the New World Order unless he or she will make a pledge to worship Lucifer. No one will enter the New Age unless he will take a LUCIFERIAN Initiation." (David Spangler, Director of Planetary Initiative, United Nations)

Kwamba, hakuna yoyote atakayeingia katika Mpango Mpya wa Dunia isipokuwa amekula kiapo cha kumwabudu shetani na hakuna atakayeingia kizazi kipya pasipo kufuata nyanyo za Lucifer, hii ni kwa mujibu wa David Spanler, Mkurugenzi wa Mpango wa Sayari, Umojan wa Mataifa.

Wakati Jamii ya siri ijulikanyo kama Illuminati ilipohusika kumuua Rais wa Marekani John  Kennedy, walifanya hivyo kwa mujibu wa namba ya maangamizi,   namba 11. Aluawa mwezi wa 11 siku ya tarehe 22 ukijumlisha unapata 33 ambayo ni daraja la juu la Freemasons.

Aliuawa kwenye himaya ya Freemasons, Masonic Dealey Plaza, jamii yenye nguvu kuliko hapa duniani inayoamini sana namba 11.

· Namba kuu ‘The Master Number’

Namba 11 huwakilisha maono, namba 22 huwakilisha maono na vitendo, namba 33 huongoza dunia na hizo ndizo namba kuu tatu kubwa zaidi ambazo zinatengeneza PEMBETATU yenye maelezo ya ufafaunuzi wa siri “A triangle of enlightenment” au “ illumination”.

Julai  6, 1946 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa George Bush (mwana), siku hiyo ikikokotolewa inakuwa hivi, 7/6/1946 = 7 + 6 = 13, 1946 = 1 + 9 + 4 + 6 = 20. 20 + 13 = 33 .. .. 11 + 22. George ni mwanachama wa jamii ya siri ya Skull and Bones (a spin-off of the Brotherhood) kama alivyo baba yake na babu yake pia.

* Namba 11  ni  namba kuu yaani 'master number' au namba ya nguvu 'power number', namba isiyogawanyika kwa mbili wala tatu, kwa Freemasons wanaamini kuwa, namba 11 inahusishwa na nguvu kwamba ni kiumbe kilicho nje ya sayari hii kinachotawala ulimwengu wote.

Kimsingi shambulizi la Septemba 11 lilipangwa ama kwa kutaka Marekani kuingia vitani au kwa nia ya kuharibu uchumi. Hii inasadikisha kutimilizika kwa Mpango Mpya wa Dunia.


Ishara za mikono kumtukuza Shetani.

Wote Bill Clinton na George Bush ni Freemasons
   

Kumbuka kwamba, Marekani inapopigana vita yoyote ujue kwamba vita hiyo imepangwa muda mrefu tu, jambo au tukio lolote kubwa linapotokea katika ulimwengu huu hasa katika ardhi ya Marekani ujue kwamba jambo hilo limepangwa muda mrefu.

Siku ya kuzaliwa kwa George W. Bush ni sawa na namba 33, daraja la juu la Fremasons, na ni yeye aliyetoa amri kwamba bendera zipepee nusu mlingoti hadi September 22! Sept. 22 ni siku 11 tangu kutokea kwa tukio na hiyo inakamilisha eneo la Pembetatu la namba 11, 22, 33. Namba 9 inaachwa kwa sababu ni namba takatifu ya Illuminati.

5/5/1776 ndipo Illuminati ilipozaliwa au kuanzishwa na kihesabu zao inakuwa hivi 5 + 1 + 1 + 7 + 7 + 6 => 27 = 2 + 7 = 9. Msomaji mmoja wa makala haya anayeishi Kigamboni aliuliza kuhusu namba 9, tutaelezea namba hii kwa undani katika makala zijazo.



No comments:

Post a Comment