Na Mwajuma Juma, Mnazimmoja
WIZARA ya Afya Zanzibar imeombwa kusaidia utoaji wa dawa vijijini ili kuweza kuwasaidia wagonjwa mbalimbali ambao wanatibiwa bila kupatiwa dawa.
Ombi hilo limetolewa na Msimamizi wa Huduma kwa watu wenye Ulemavu, Bi.Raya Khamis Ali baada ya kufanya ziara katika Kitengo cha Akili na Viungo cha Hosiptali ya Mnazimmoja Wilaya ya Kusini Unguja.
Alisema, pamoja na kuwa wamekuwa wakifanya ziara kwa ajili ya kutoa huduma kupitia vijiji mbalimbali, lakini huduma hizo zimekuwa zikifanyika pasipo wagonjwa hao kupatiwa dawa.
"Hadi sasa zoezi hilo limekuwa likifanyika, lakini wanaohudumiwa huishia kupewa ushauri nasaha pekee badala ya kupatiwa dawa za kujitibu,” alisema.
No comments:
Post a Comment