13 January 2012

WATU watatu wamefariki jijini Dar es Salaam katika matukio tofauti

Na Zena Mohamed

WATU watatu wamefariki jijini Dar es Salaam katika matukio tofauti,likiwemo la watoto Swahiba Mussa (6) na Salima Rashid (5),wakazi wa Mbweni Teta kutumbukia kwenye kisima  cha maji cha asili.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charlse Kenyela alisema,watoto hao walikuwa wanacheza karibu na kisima hicho ghafla walitumbukia na kufariki baada ya kunywa maji mengi.

Kenyela alisema maiti za watoto hao ziliopolewa na wananchi wa eneo  hilo na kuhifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.

Katika tukio jingine mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Bunju Bw.Hamza Somba (18),mkazi wa Tegeta Msichoke amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya manila.

Kamanda kenyela alisema marehemu aliitundika kamba hiyo kwenye dali,sababu za kifo chake  hakijajulikana kwasababu hajaacha ujumbe wowote na maiti imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi. 

   

1 comment:

  1. Wazazi au walezi w anaji kausha lakini ukweli ni kwamba mtoto huyu amejiua kuepuka mateso anayo kumbana nayo kila siku toka kwao. Kwa vile ushahidi umekufa, watajifanya hawajui sababu ya kifo chake lakini Mungu atawahukumu juu ya unyanyasaji wao huo.

    ReplyDelete