13 January 2012

Wafanyabiashara waomba mfumo wa ushuru

Na Damiano Mkumbo
Singida

WAFANYABIASHARA wa mji wa Singida wameishauri Halmashauri ya Manispaa hiyo kuwapa mfumo mzuri wa kukusanyaji wa ushuru mbalimbali ili kuondoa usumbufu.


Ushauri huo ulitolewa katika taarifa yao iliyowasilishwa katika Ofisi ya Chama cha
Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima mkoani Singida.


Akizungumza kuhusu suala hilo juzi Ofisa Mtendaji wa Chama hicho Bw. Calvert Nkurlu alisema kuwa wajasirimali hao wamesema kuwa mfumo mzuri utaweza kurahisisha ukusanyaji wa ushuru kuliko ilivyo sasa  na kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima.


Alisema kuwa ni vema kuweka pamoja ushuru unaofanana na kupunguza idadi ya wakusanyaji, kwani mfanyabiashara moja hufutwa na watu watano wakidai ushuru wataka, ushuru wa huduma, mabango au maegesho ya magari.

Alisema kuhusu mazingira ya kazi, alisema kuwa wafanyabiashara wa eneo hilo wamekuwa wakifanya shughuli zao katika hali nzuri kutokana na kuwa na uhusiano mzuri kati yao na Manispaa hiyo pamoja Mamlaka ya Kodi mkoani humo.

Bw. Nkurlu alisema hali hiyo imetokana na chama hicho kuondoa vikwazo vilivyokuwepo zamani na kutoa elimu ya ujasirimali na Elimu ya mlipa kodi kwa
wanachama wake.

Hata hivyo, aliwashauri wafanyabiashara kuendelea kujiunga kwa wingi katika chama hicho ambacho ndiyo chombo pekee cha kuwaunganisha na kuwatetea.

Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima mkoani Singida kina jumla ya wanachama 500 wakiwemo katika Halmashauri zote nne za Singida, Iramba, Manyoni na Manispaa ya Singida.

No comments:

Post a Comment