13 January 2012

Chama cha ushirika chatoa mkopo mil 572.4/-

Na Damiano Mkumbo
Singida

CHAMA cha Ushirika wa Akiba na mikopo cha Tumaini Manyoni mjini kimetoa mikopo yenye thamani  ya zaidi ya shilingi milioni 572.4 kwa wanachama wake katika kipindi cha kuanzia mwaka 2004 na 2011.


Taarifa hiyo ilitolewa na Meneja wa chama hicho Bw. Yohana Samwel Malogo alipokuwa kizungumzia  maendeleo ya SACCOS hiyo juzi.

Bw.Malogo alisema mikopo hiyo iliwawezesha wanachama kuendeleza kilimo, Biashara, kujenga nyumba bora na kulipia ada za watoto wao wanaosoma katika shule za sekondari na Elimu ya juu.

Meneja huyo alibaini kuwa kati ya fedha hiyo jumla ya shilingi  milioni 384.2
zimerejeshwa na kingine kilichobaki kitarejeshwa kulingana na muda
aliyepangiwa mkopaji.


Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2011 chama hicho kilitoa mikopo yenye jumla ya shilingi milioni 223.5 kwa wanachama 197 wakiwemo wanawake 101 na wanaume 96 pamoja na vikundi 10 vya wajasiriamali.

“Tumejenga uwezo wa wanachama katika kuongeza uzalishaji kwa njia ya kilimo kwa
kuwakopesha zana za kilimo yakiwemo matrekta makubwa 13 na moja dogo aina ya 'Power tiller'  kwa ajili kuondokana na matumizi ya jembe la mkono katika kuinua uchumi wao," alisema.


Alisema mikopo hiyo imetokana na Benki ya Uwekezaji ya Tanzania (TIB) ilitoa kwa
Chama cha Ushirika wa Akiba na mikopo cha Tumaini mjini Manyoni ya shilingi milioni
168.2 wenye masharti nafuu, ambapo riba yake ni asilimia 8 kwa mwaka.

Alisema chama hicho kina mtaji wa shilingi milioni 141.7 zikiwa ni
hisa, akiba na hisa za wanachama, na kuongeza mtaji huo kutoka nje kwa kupata mikopo yenye thamani ya sh. milioni 1900 kutoka Benki ya CRDB na Pride Tanzania.

Chama hicho kilichoanzishwa mwaka 2004 kwa jina la Anglican SACCOS na kubadilishwa jina kuwa Tumaini kikiwa na wanachama 74 sasa kina jumla ya wanachama 540 wakiwemo wanawake 294 na wanaume 232, vikundi 11 na wateja 3.

No comments:

Post a Comment