13 January 2012

Ulinzi Shirikishi

Na David John

JESHI la Polisi Mkoa wa kipolisi Temeke limesema kuwa katika kuimarisha suala zima la Ulinzi shirikishi limukusudia kuazisha Uperesheni fufua, imarisha vikundi vya ulinzi shirikishi ili kupambana na uharifu.

Akizungumza na majira Dar es salaamu jana Kamanda wa Mkoa huo Bw. David Misime alisema kuwa lengo la kuazisha uperesheni hiyo ni kutaka kusafisha vitendo vyote vya uharifu katika Wilaya hiyo.

Alisema kuwa jeshi la polisi haliwezi kufanya kazi pekee yalke bila kuwepo kwa makundi hayo na kufanya hivyo itakuwa ni uwepesi polisi kubaini uhalifu kupitia msaada wa makundi hayo.

"kazi ya kupambana na uhalifu katika Wilaya yetu na nchi kwa ujumla haiowezi kuwa ya polisi pekee lazima jamii kupitia ulinzi shirikishi ishirikiane na jeshi la polisi katika kufichua wa harifu"alisema Kamanda Misime.

Aliongeza kuwa ili kupambana na uhalifu lazima jamii husika kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi lakini kinyume na hapo hatuwezi kufanikiwa katika kusafisha Wilaya ya Temeke

 "temeke lazima jamii zetu zinazo tizinguka sisi sote kwa pamoja tushirikiane ndiyo tutaweza kufanikisha malengo haya"alisema

Alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni jamii kuwa na hulka ya kufanya maamuzi mkononi bila kufuata sheria zilizopo na hatua hiyo inahatarisha maisha ya watu katika jamii.

 Alisema binadamu wamekuwa na hulka ya kutokubali kubadilika na kutam,bua ulinzi na usalama siyo tu ni jukumu la jeshi la polisi hilo nalo ni tatizo kwa wananchi :kuna haja ya kuendelea kuielimisha jamii kutambua majuku yao katika kulinda Taifa lao"alisema Kamanda Misime.

Alisema tukio linapokuja halina mwenyewe hivyo lazima wote kuwa walinzi katika jamii ,nakufanya hivyo kutawezesha kupunguza matukio hasa katika jiji la Dar es salaama pamoja kuwa hali kwa sasa siyo mbaya.

No comments:

Post a Comment