Serikali, madaktari wafikishana pabaya
*Sasa wapashana kupitia vyombo vya habari pekee
*Wagonjwa wataabika, ndugu wahaha kuwahamisha
*Watangaza athari za mgomo ndani ya siku 12
Anneth Kagenda na Rehema Maigala
WAKATI afya za wagonjwa wanaotibiwa katika
hospitali mbalimbali nchini zikizidi kudhoofika kwa
kukosa matibabu, kwa mara nyingine tena madaktari
na serikali jana wameendelea kutunishiana misuli,
hali inayodhihirisha kuwa muafaka wa sakata hilo
bado kitendawili.
Hali hiyo ilijidhihirisha Dar es Salaam jana wakati
umati mkubwa wa madaktari hao ulipojikusanya kwenye
mkutano wa hoteli moja jijini, na kutoa tamko la
kutorudi nyumba, huku wakisisitiza kuwa matokeo ya
mgomo wao yataanza kuonekana siku 12 zijazo na
kuendelea.
Wakati madaktari hao wakitangaza msimamo wao huo,
siku hiyo ya jana maofisa waandamizi wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii wakiongozwa na waziri wao,
Dkt. Hadji Mponda, walikutana na waandishi wa
habari na kutoa majibu ya madai yao ambayo
hayaoneshi nuru ya kumaliza mgogoro unaoendelea,
bali kukuza ukubwa wa tatizo.
Pamoja na Dkt. Mponda kuwaambia waandishi wa habari
jana kuwa milango ya wizara yake ipo wazi tayari
kwa kukutana nao, madaktari hao nao walijibu kuwa
mgomo unaendelea hadi pale watakapokutana na Waziri
Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, au ujumbe kutoka ofisini
kwake.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es
Salaam jana Mwenyekiti wa Jumuiya Mpya ya Madaktari
Dkt. Steven Ulimboka, alisema mgomo bado upo pale
pale na kwamba wao wanamtaka Waziri Mkuu Bw.
Pinda.
"Tunachosema ni kwamba milango iko wazi kwa
ajili ya mazungumzo na serikali, lakini serikali
iache kupotosha umma kwamba hakuna mgomo, ukweli ni
kwamba mgomo upo pale pale hadi kieleweke,"
alisema, Dkt. Ulimboka
Aliongeza kuwa hivi karibuni walikutana na uongozi
wa juu katika ofisi ya Waziri Pinda ambao ni Katibu
na Naibu Waziri, na kuzungumza nao kwa saa tatu,
lakini walishindwa kufikia muafaka, hatua
iliyosababisha mgomo kuanza.
"Serikali iache propaganda kwani kuna kamchezo kanachezwa, ndiko kanakowafanya wazunguke zunguke, hawana jibu moja la kutujibu, badala yake wanaitisha mikutano na
vyombo vya habari... kwanini wasije kuzungumza na
sisi ili muafaka upatikane?"Alihoji Dkt.
Ulimboka.
Alisisitiza kuwa; "Sisi tunachokifanya
tuko sahihi na wala hatujakosea, kama wao wanasema
tutafika mahali tushindwe hiyo si kweli, ila
waache siku ziendelee kusogea mbele na ikifika siku
ya 12 na kuendelea majibu yatapatikana katika
hospitali zote nchini."
Alisema madaktari watashangaa ikiwa watapata
taarifa kwamba Waziri Pinda anasafiri wakati
wananchi wanaendelea kufa hospitalini, eti kwa
madai kuwa serikali imeshindwa kufikia muafa na
wao.
Wakati madaktari wakitoa msimamo huo, Dkt.
Mponda naye alikuwa na waandishi wa habari
akipangua kwa majibu hoja nane za msingi
zilizofikishwa na madaktari hao mezani kwake ili
zijadiliwe na hatimaye waweze kurejea kazini.
Alianza kwa kutoa mwito kwa madaktari ambao wapo
kwenye mgomo, kuacha mara moja ili kunusuru maisha
ya Watanzania wanaofika hospitalini kwa ajili ya
kupata tiba.
"Ni vyema madaktari wakatambua juhudi zinazofanywa
na serikali za kuboresha maslahi ya Sekta ya Afya
na wanatakiwa kuziunga mkono, hivyo basi tunawasihi
kurejea kazini", alisema Dkt. Mponda.
Katika hatua nyingine serikali imekiri mgomo huo kusambaa katika baadhi ya mikoa ingawa badohainataarifa ya athari zake.
Wakati huo huo waandishi wetu waliotembelea
baadhi ya hospitali mbalimbali jijini na mikoani,
wameshuhudia baadhi ya ndungu wakifanya mipango ya
kuwahamishia wagonjwa wao hospitali za binafsi.
"Ndugu yangu hali ni mbaya, sielewi tunaenda wapi
hapa hospitali (Muhimbili) hakuna madaktari
tunaambiwa wapo kwenye mikutano wamegoma, ni bora
tuhamishe wagonjwa wetu tuwapeleke nyumbani,kwani
wengine hatuna kipato cha kuhamishia hospitali
binafsi," alisema.Mhudumu wa chumba cha kuhifadhi
maiti katika hospitali ya Muhimbili alipoulizwa
kama vifo vya wagonjwa vimeongezeka tangu mgomo huo
uanze, alijibu huku akitabasamu; "Hiyo siri ya
jeshi, lakini simama hapa mwenyewe uanze kuhesabu
zitakazoletwa.
"Mitaani nako walionekanakusikitika pale walipokuwa wakipitwa na magari ya wagonjwa (Ambulance) yakipiga ving'ora wakati wanakopelekwa kwa ajili ya matibabu ya juu zaidi madaktari wamegoma.
Wakati huo huo; taasisi inayojishughulisha na masuala ya afya na elimu kwa jamii nchini (SIKIKA) imeitaka wizara hiyo kuchukua hatua za haraka kumaliza mgogoro huo, ili
kuepusha madhara makubwa yanayoendelea
kujitokeza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa jana
kwa vyombo vya habari na SIKIKA ilifafanua kuwa
wizara ina jukumu la kushirikiana na madaktari ili
kuboresha afya za wananchi.
"Ijulikane kuwa, jukumu la awali la wizara kwa kushirikiana na madaktari ni kuboresha afya za wananchi na kuokoa maisha yao, hivyo ni wajibu wao kufanya kazi kwa pamoja ili kufanikisha hili," ilisema taarifa na kuongeza.
Naye Mashaka Mhando,anaripoti Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Bw. Evarist Ndikilo, amesema
madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani
hapa, hawajaanza mgomo kama wenzao katika baadhi ya
mikoanchini, isipokuwa wanaweza kuungana nao
kuonesha mshikamano.
Hata hivyo alisema ofisi yake
imeongea nao kuona uwezekano wa kuepusha mgomo huo.
Akizungumza na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
iliyokuwa na ziara mkoani hapa, alisema madaktari
wa hospitali hiyo na zingine zilizopo mkaoni hapa,
wanaendelea na kazi na wala hawajagoma kama
wengine.
bugando wamegoma
ReplyDeleteSilikari iache kususuasua, iwalipe hao madakitari alaka sana. Figogo wa selikali finajilipa malupulupu menge pamoja na posho nyingi za mikutano isiyokuwa na ulazima wala tija. Alafu wabunge nao wanajiripa posho maradufu. Na wote hao wakiugua hata mafua wanakwenda kutibiwa majuu kwa pesa nyingi za waripa kod na walalahoi. Magari ya kifahali ya silikari makubwa ya pesa nying wana ela ya kununulia lakini hawana za kuongeza mishaala ya madakitari. Iyo ni akiri? Aiingia kichwani ata kidogo. Madakitali, waambie waripe kwanza ndo mtoe uduma.
ReplyDeleteWatanzania tufike mahali tumtambue adui yetu. Kwa kweli haingii akilini kuona wabunge wenye utitiri wa posho wakipandishiwa posho ambayo hata wao walishangaa, harafu serikali inashindwa kuongeza masilahi ya madaktari!. Hivi ni vipi mawaziri wa afya walishindwa kufika Don Bosco kuongea na madaktari kabla ya mgomo kuanza? wakati jana baada ya mgomo kuleta athari wakaweza kufika hapo starlight!!!!!!!!. Hawa viongozi hawatusaidii ila wapo kwa masilahi yao binafsi.
ReplyDeleteunajua taaluma ni ki2 muhimu cna maishani mwa binadamu na unaweza mtu ukafanya kazi sehemu yeyote ile dunian bila bugudha ya mtu wa wala wanaohitaji huduma yako bali kwa sisi serikali yetu sio wazalendo kwan nan na ana nguvu gani kwa kazi ipi na alipwe mshahara mnono mbunge bila kuwa na kazi muhim katika jamii au huyo jaji mkuu au majaji wenzake wanakazi ipi muhimu katika kuokoa maisha ya watanzania moja kwa moja,tazama mara mbili naunga mkono moja kwa moja mgomo wa madakitari,solidarity forever
ReplyDeletehivi hawa mawaziri pamoja na rais wao wanpepo gani ambao wanahitaji waombewe ndio hawatoke ona kiranja wao mkuu kaenda kuuzulia mkutano wa nchi 20 tajiri ikiwa sis ni top ten ya mwisho na kwa kutumia takribani 300millions za walipa kodi wengi wao ni maskini na tunaishi chini ya dora moja this is not true then lets put all a side and pray for a god to save us,naomba mdingatie taaluma za watu ambao wameangaika darasi kwa muda mrefu arafu leo umunyonye noooo,tukiwa chuo/shule tunavumilia vya kutosha na huku nako
ReplyDeleteCHONDE CHONDE PINDA KAMA KWELI UNAFANYA KAZI FUKUZA MAWAZIRI WAZEMBE NA WATENDAJI WOTE WA SERIKALI,ULISEMA HATA POSHO ZA WABUNGE NI NDOGO:
ReplyDeleteMADAKTARI ENDELENI NA MGOMO KWA HAO WANAOWAFUKUZA WANATIBIWA INDIA HAWANA SHIDA ETI.
PINDA TANZANIA YA LEO SIYO ILE YA ZAMANI ETI
KUFUKUZANA SIYO JAWABU LA KUTIBU WAGONJWA,TANZANI TUNASHIDA YA MADAKTARI, LAZIMA TUJIULIZE KWANINI WANAGOMA?
Mh. Pinda mbona unatumia mabavu wakati swala la madaktari linajulikana? Hapa sio mahala pa kutumia nguvu kwani madaktari wa interns walifukuzwa ndio balaa likaanza na wewe unamwagia moto petroli, kaa na hao madaktari mujadili kwa kina jinsi ya kuwatatulia matatizo yao ukimalizana nao lazima watarudi kazini... Shida yao ni kusikilizwa na yale ya muhimu yatimizwe acheni utemi damu itamwagika na sisi wananchi wa kawaida ndio tutapata shida... Mungu awaongoze katika kutoa maamuzi..
ReplyDeleteKama ziko za kuwalipa posho wabunge kwanini wasiwalipe madaktari na wauguzi? Haiingii akilini kuona viongozi wetu wanafanya ukatili na uonevu wa aina hii. Madaktari na wauguzi msimamo wao uwe pale pale. Viongozi wasidhanie wanaweza kuwatisha. Ni lini hawa wenda wazimu watakuwa sober na kusikiliza vilio vya wananchi na wanataaluma?
ReplyDeleteHivi wanaharakati wa haki za binadamu mnatushaurije sisi wananchi? Tunaweza kuishitaki serikali kwa uzembe na kutowajibika kulikosababisha vifo na hasara za kibinadamu kutokana na matatizo haya? Tupeni ushauri jamani. Tuishitaki serikali itulipe fidia. Washike adabu kufanya dharau na ujeuri kwa maisha ya watu. Lazima hii serikali dhalimu iwajibishwe.
ReplyDeleteHivi wanataka kutuambia hakuna pesa za kulipa madakatari haki zao,pesa zinaishia tu kwenye mambo ya siasa,ushabiki wa siasa.majuzi wamemaliza mabilion kwa ajili ya miaka 50 ya uhuru,mabilioni ya changuzi ndogo igunga,pesa za rada zikarudishwa zimeenda wapi mbona yalikuwa mabilioni.madaktari walipwe,walimu walipwe,na wote wenye madai sugu,serikali wanajinufaisha wenyewe mkomae.wao wanatibiwa india,na regency,agakhan hindmandal.wanasababisha vifo kwa umafia wao.pesa zipo,zitoke.ngoja watangaze uchanguzi wa majimbo yaliyowazi,wataona reaction za walala hoi.haiwezekani wanakaa tu kimya.huko bungeni wamefuata posho wala si kujadili.wanaacha watu wanakufa wanaenda kujadil miradi ya nani na watu wenyewe wanakufa?
ReplyDelete