27 January 2012

CHEKA,NYILAWILA KUPIMA UZITO LEO.

Na Mwali Ibrahim

MABONDIA Karama Nyilawila na Francis Cheka leo wanatarajia kupima uzito kwa ajili ya kujiandaa na pambano lao lisilo kuwa la ubingwa linalotarajia kufanyika kesho.

Pambano hilo la raundi 10 uzito wa kg 75 linatarajia kufanyika katika uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro.

Katika pambano hilo pia kutakuwa na mapambano mengine makubwa matano yakisindikiza pambano hilo ambalo ni kati ya Maneno Osward 'mtambo wa gongo'na Pasco Ndomba raundi nane uzito wa kg 75, Chaulembo Palasa na Deo Njiku kg 68.

Wengine ni Venance Mpoji na Ibrahim Clases kg 63, Anthon Mathias na Juma Afande kg 54 na pambano la mwisho kati ya Hassan Kidebe na Arbert Mbena kg 54 ambapo mapambano hayo yatakuwa ya raundi sita kila moja.

Wakizungumza kwa njia ya simu kutoka Morogoro Cheka alisema, tayari wameishapima UKIMWI na amekutwa yupo sawa na hivyo anasubiri vipimo vya mwisho ambavyo vitaenda sambamba na upimwaji uzito.

Akizungumzia maandalizi yake kwa ujumla alisema, yupo tayari kwa kupanda ulingoni na anauhakika wakufanya vyema na kuacha ushindi mkoani humo ikiwa ni kama shukurani ya kumsapoti.

"Mimi nasubiri muda tu ufike nimepima UKIMWI nipo sawa na maandalizi pia nipo sawa sasa kilichobaki ni kusubiri muda wa kupanda ulingoni tu na kuweza kuchukua ushindi," alisema Cheka.

Naye kwa upande wake Nyilawila alisema, raundi hizo 10 ndio zitaamua nani mshindi kwani kama alivyosema hana kwa waida ya kupigwa ugenini hivyo nilazima aendeleze historia  yake.

"Hata kama tukimaliza raundi zote lazima ni nyakuwe ubingwa hivyo raundi 10 zitaamua nani bingwa," alisema.

No comments:

Post a Comment