19 January 2012

RT yasogeza mbele Uchaguzi Mkuu

Na Andrew Ignas

SHIRIKISHO la Riadha nchini Tanzania (RT) limesogeza mbele tarehe uchaguzi
ambao ulipangwa kufanyika Machi 14 hadi 15, badala yake sasa utafanyika  Machi 16 hadi 17 mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu  Mkuu wa RT, Suleimani Nyambui alisema Kamati ya Mashindano ya chama hicho imeamua kuusogeza mbele kutokana na fomu za wagombea kuchelewa kutoka.
"Kamati ya Utendaji imesogeza mbele tarehe ya uchaguzi ambao awali ulipangwa kufanyika Machi 14 hadi 15 mwaka huu, kutokana na fomu za wagombea kuchelea kutoka," alisema Nyambui.
Alisema nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huo ni Rais, na Makamu wake wawili mmoja wa Kamati Utendaji na mwingine wa Utawala.
Nyambui alisema nafasi nyingine ni Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini na Wajumbe 10 wa Kamati Utendaji.
Wakati huohuo, Katibu huyo amewataka wadau mbali mbali wa riadha wajitokeze kugombea nafasi hizo.

No comments:

Post a Comment