LUANDA,Angola
MCHEZAJI Nando Rafael ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Angola kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika, lakini huenda hasicheze kwenye fainali hizo za mwezi huu zitakazofanyika katika nchi za Guinea ya Ikweta na Gabon.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), pamoja na mchezaji huyo kutajwa kwenye kikosi hicho lakini Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) bado halijatoa kibali kwa mchezaji huyo kuichezea Angola.
BBC ilieleza kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 tayari alishaichezea timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 21 ya Ujerumani, hivyo anahitaji kibali maalumu kutoka FIFA.
Hata hivyo FIFA ilisema hadi jana, ilikuwa haijapokea maombi yoyote ya Angola ya kumtumia Rafael katika michunao hiyo.
Kikosi cha Angola, kilichotaja majina yake Jumamosi, kilitakiwa kuwasilishwa CAF katikati ya wiki iliyopita.
Katika kikosi hicho, Kocha Lito Vidigal, amemuita beki Kali na washambuliaji Flavio na Love, ambao wamewahi kuichezea Angola kwenye fainali tatu zilizopita.
Angola, ambayo mwishoni mwa wiki ilikuwa ikicheza mechi yake ya mwisho ya kujiandaa na michuano hiyo dhidi ya timu ya Sierra Leone,mjini Cabinda,imepangwa Kundi B ambapo itakutana na timu za Taifa za Burkina Faso, Ivory Coast na Sudan.
Kikosi kamili kilichotangazwa na kocha huyo ni kama ifuatavyo,walinda mlango ni Carlos, Hugo (Kabuscorp), Wilson (Primeiro Agosto).
Mabeki Amaro, Dani Massunguna na Kali (wote Primeiro Agosto), Marco Airosa (AEL Limassol, Cyprus), Mingo Bille (Primeiro Agosto), Zuela (Atromitos, Ugiriki)
Viungo Andre Makanga (Al Jahra, Kuwait), Dede (AEL Limassol, Cyprus), Gilberto (Lierse, Ubelgji), Mabina, Miguel (wote Petro Atletico), Osorio (Recreativo Caala), Xara (Petro Atletico)
Washambuliaji ni Djalma (FC Porto, Ureno), Flavio (Lierse, Ubelgji), Jose Pierre Vunguidica (Preussen Munster, Ujerumani), Love (Petro Atletico), Manucho (Real Valladolid,Hispania), Mateus Galiano (Nacional, Ureno), Nando Rafael (FC Augsburg,Ujerumani).
No comments:
Post a Comment