16 January 2012

Mtoto wa Wacko Jacko aanza 'mbwembwe'

LAS VEGAS, Marekani

WAHENGA walisema mtoto wa nyoka ni nyoka.

BINTI wa mwanamuziki aliyekuwa mfalme wa Pop, Michael Jackson (Wacko Jacko), Paris ameonekana kuanza kufuata nyayo za baba yake kwa kuigiza uchezaji wake ikiwemo mtindo wa kusimama kwa kutumia vidole vya mguuni wakati akicheza mpira wa magongo.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, katika Uwanja wa shule akicheza mpira wa magongo binti huyo mwenye umri wa miaka 13 alionekana akiwa amesimama kwa kutumia vidole na kutembea kama baba yake alikuwa akicheza muziki jukwaani kwa mtindo huo.

Jackson alifariki Dunia Juni 25, 2009 kutokana na kuzidisha dozi ya dawa za kupunguza maumivu.

Kutokana na kifo chake daktari wake, Conrad Murray  alishitakiwa kwa kusababisha kifo chake na tayari ameshahukumiwa kifungo cha miaka minne.

No comments:

Post a Comment