18 January 2012

MECKI kuchaguana Januari 28

Na Martha Fataely, Moshi
KLABU ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kilimanjaro (MECKI),
inatarajia kufanya mkutano mkuu maalum ambao utahusisha mabadiliko ya katiba ya klabu hiyo na uchaguzi wa katibu mkuu. 
Mkutano huo utakaohusisha wanachama wa klabu hiyo utafanyika mapema Januari 28, mwaka huu. Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Nakajumo James, alinukuliwa katika barua yake kwa wanachama wa klabu hiyo kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika Mjini Moshi kuanzia saa 3.00 asubuhi.
Alisema uchaguzi huo unafanyika ikiwa ni baada ya aliyekuwa Katibu wa klabu hiyo, Bw. Yusuph Mazimu, kujiuzulu nafasi hiyo na kuajiriwa kuwa mratibu wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC).
“Uchukuaji na urejeshwaji wa fomu kwa ajili ya uchaguzi ni kuanzia Januari 13 hadi  21, fomu zitapatikana ofisini MECKI kwa
kufuata utaratibu uliopo wa kulipia sh. 10,000 kwa nafasi za juu na shs. 5,000 kwa nafasi ya ujumbe,”ilieleza sehemu ya barua hiyo.
Kuhusu marekebisho ya katiba katibu huyo alisema yanafanyika ili kukidhi mahitaji ya sasa na kwa kufuata maazimio ya mkutano mkuu wa UTPC wa Septemba 12 na 13 mwaka jana.
Mkutano huo ulizitaka klabu za waandishi wa habari nchini kufanya marekebisho ya katiba kabla ya Februari, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment