18 January 2012

Dawa bandia za malaria zaongeza madhara

LONDON,Uingereza

WANASAYANSI  katika Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza
wamesema kuwa ongezeko la dawa bandia barani Afrika, ni pigo kubwa katika juhudi zinazoendelea za kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Habari kutokajijini Londan zinaeleza kuwa wanasayansi wa chuo hicho walisema juzi kuwa kuuzwa kwa dawa hizo bandia huwadhuru wagonjwa mbali mbali na kusababisha wagonjwa hao kutoweza kupata tiba kamilifu wanapotumia dawa sahihi.
Wataalamu hao wa dawa walisema baadhi ya dawa hizo bandia zinatoka nchini China.
Wameshauri kuwa wataalamu wa masuala ya afya katika bara la Afrika wanapaswa kuchukua hatua kambambe za kusitisha kuenea kwa dawa hizo bandia katika bara la Afrika au sio mamilioni ya watu watafariki.
Kwa mujibu wa wataalamu hao waathirika wengi wa dawac hizo  bandia ni watoto na wanawake waja wazito.
Shirika la la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO),linakadilia kuwa watu wapatao milioni moja upoteza maisha kila mwaka baranin Afrika kutokana na ugonjwa huo wa Maralia.(BBC)

No comments:

Post a Comment