Na Grace Ndossa
MAHAKAMA Kuu kanda ya Dar es Salaam itaanza kusikiliza kesi ya kumshikilia aliyekuwa mgombea urais nchini Burundi Bw. Alex Sinduhije Febuari 6 mwaka huu.
Uamuzi huo ulitolewa jana mahakamani hapo na jaji Laurence Kaduri baada ya mawakili wakuu wa serikali Bw. Obed Kameya na Bw. Edwin Kakolaki walipofika mahakamani kwa ajili ya kuwakilisha mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Ofisi ya mwanasheria Mkuu
wa serikali.
Wakili wa serikali Bw.Obed Kameya aliieleza mahakama kuwa walipata amri ya kuitwa mahakamani jana mchana, hivyo wanaomba wapewe muda wa siku saba ili waweze kujibu madai hayo.
Jaji Kaduri alikubalina na ombi hilo na kutoa muda wa siku saba wawe wamejibu kwa njia ya maandishi hadi 31 januari wawe wameshajibu.
Hata hivyo wakili anayemtetea Bw. Senduhiji Bw. Hurbet Nyange atatoa majibu ya nyongeza februari 3 mwaka huu.
Bw. Sinduhiji alikamtwa katika uwanja wa ndege wa Kimatifa wa Mwalimu Julias Nyerere kwa hati ya shirika la polisi la kimataifa la (Interpol)akitokea Uganda kluja Nchini na Januria 13 alifikishwa mahakamani kisutu lakini hakusomewa mashtaka.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi na kushikiliwa na polisi kwa siku mbili mfululizo katika kituo cha polisi kati Dar es Salaam huku kukiwa hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini na jeshi hilo kuhususababu za kukamtwa kwake.
Wakati akikamatwa na Interpol Bw. Sinduhiji alituhumiwa na serikali ya burundi kuhusika na mauaji ya mwakili wa shirika la afya la umoja wa Mataifa(WHO)Dkt KassiManlan raia wa Ivory coast na aliyekuwa mtumishi wake na pia mauaji ya halaiki ya katumba.
No comments:
Post a Comment