25 January 2012

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam-yatoa Amri

Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa amri ya kuitaka ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali na ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kufika mahakamani hapo kwa ajili ya kuieleza Mahakama hiyo uhalali wa kumkamata na kumshikilia aliyekuwa mgombea urais nchini Burundi Bw.Alex Sinuhnje (46).
Amri hiyo ya mahakama imetolewa jana mahakamani hapo na Jaji Lowlance Kaduli iku moja baada ya wakili anayemtetea Bw.Sinduhnje,Bw.Hurbet Nyange juzi kuwasilisha ombi linalotaka mahakama hiyo itowe amri ya kuachiwa huru kwa mteja wake.

Jaji Kaduli alitoa  amri hiyo akitaka wawakilishi wa ofisi hizo kufika mahakamani hapo saa 3 asubuhi leo kwa ajili ya kutoa maelezo hayo.

Ombi lililowakilishwa Mahakamani hapo juzi na Bw.Nyange ni namba 7/2012 ambapo Bw.Sinduhnje anamshitaki Mkuu wa Jeshi la polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa serikali kwa kile anachodai kuwa mteja wake ameshikiliwa kwa muda wa siku 14 bila ya kufikishwa mahakamani.

Habari kutoka nje ya mahakama kutoka kwa wakili wake Bw.Nyange zilidai kuwa Bw.Sinduhnje aliwaeleza polisi kuwa yeye ndiye aliye andika habari za kifo cha Dokta Kassy Leopad wa Shirika la Afya Duniani (WHO) akiwa kama mwandishi wa habari za uchunguzi na kusababisha watuhumiwa wa mauwaji hayo kukamatwa

 Alidai kuwa wakati mauwaji hayo yanatokea Novemba mwaka jana yeye alikuwa nchini Ufaransa.

Hata hivyo Bw.Nyange alidai kuwa kwa kawaida serikali ya Burundi ilipaswa kuleta ushahidi wa kuonesha kuwa Bw.Sinduhnje ni mshtakiwa nchini humo jambo ambalo halikufanyika licha ya kukamatwa nchini.

Alidai kuwa yeye kama wakili wake amepata mkanda wa video kutoa nchini Burundi unaoeleza kuwa serikali ya nchi hiyo haikutoa maelekezo ya mteja wake kukamatwa kama ilivyofanyika.

Januari 13 mwaka huu ,Bw.Sinduhnje alifikishwa katika maabusu ya Mmahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lakini hakupandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka ya mauwaji aliyodaiwa kukabiliwa nayo.

No comments:

Post a Comment