21 December 2011

Wazambia kuichezesha Twiga Stars

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limeteua waamuzi kutoka Zambia kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC), kati ya
Tanzania (Twiga Stars) na Namibia.

Wambura alisema mechi ya kwanza itachezwa jijini Windhoek, Namibia kati ya Januari 13, 14 na 15 mwakani.

Alisema mwamuzi wa kati ni Gladys Lengwe wakati waamuzi wasaidizi ni Patience Mumba na Mercy Zulu.

Wambura alisema wamuzi wa akiba (mezani) atakuwa, Bookanang Lekgowe kutoka Botswana wakati Kamishna wa mechi hiyo kutoka Afrika Kusini atakuwa Smith Hilton Fran.

Alisema mechi ya marudiano itachezwa Januari 29 mwakani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Twiga Stars inayofundishwa na Kocha Charles Mkwasa akisaidiwa na Nasra Mohamed, imeanza rasmi mazoezi juzi kwa ajili ya mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment