21 December 2011

Waandamana, wavaa magunia kupinga posho za wabunge

Na Waandishi Wetu, Arusha

WANAHARAKATI wa Kikundi cha Wazalendo Associate, mkoani Arusha, jana wameandamana kwa miguu umbali wa kilometa saba wakiwa wamevaa magunia mwilini ili
kupinga nyongeza ya posho za wabunge kutoka sh. 70,000 hadi sh. 200,000.

Kikundi hicho kilidai kuwa, nyongeza hiyo imelenga kumwangamiza Mtanzania wa kawaida.

Akizungumza baada ya kumaliza maandamano hayo, mmoja wa viongozi wa kikundi hicho ambaye pia ni diwani wa Kata ya Sombetini, Bw. Aphonce Mawazo, alisema wameamua kutembea peku na kuvaa magunia ili kufikisha ujumbe huo kwa Serikali.

“Kama posho hizi zitapitishwa, muda si mrefu Watanzania wote wataungana kuvaa vazi hili kwa kuwa hawataweza kumudu gharama za maisha, tumeamua kupaza sauti kwa waliopewa dhamana kwani ubinafsi umetawala katika mioyo yao,” alisema.

Alisema kitendo cha Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda kusema wabunge wake wanaonekana ombaomba sio sababu ya msingi kwa kuwa wapo wananchi wengi mjini Dodoma ambao wanaomba bila kusaidiwa.

Bw. Mawazo alisema kama Bunge litaendelea kujadili posho na maslahi yao, watalazimka kutembea kwa miguu wakiwa wamevaa magunia hadi mjini Dodoma.

Alisema watafanya hivyo kwa lengo la kuhamasisha wananchi wengine nchi nzima kwenda Dodoma kudai na kupigania haki zao.

3 comments:

  1. Haki ya Mungu na waandamane hadi kieleweke, kwa nini Spika (Mama mjinga huyu) akingie kifua posho na uchoyo wake wa pesa na uchu wake wa madaraka akiwa hajui kazi posho hizi? Mbona asiwakingie kifua wanafunzi, watoto wa wakuliwa huko vyuo vikuu wana fukuzwa kwa kudai posho zao za mikopo zinazo tolea na kuliwa na wajanja?? Mama Makinda, Naapa kwa jina la Mungu SIKUPENDI JINZI ULIVYO NA SIPENDI KAZI ZAKO CHAFU. Anajipa madaraka ya Uraisi bila kuamriwa kufanya hivyo, masikini wanateseka na watoto majumbani kwa kukosa karo, hatuna hata sukari vijijini na hatuna hata mafuta ya taa maana hatuwezi kuyanunua, yeye anajilipa pesa nyingi ambazo ni jasho letu, Ashindwe na alegee, hafai, mlimtoa wapi huyu kibwengo jamani??

    ReplyDelete
  2. mi nashangaa, angalia wastsafu waliotumikia wananchi kwa miaka mingi na waadilifu lakini wanalipwa shs 50000/= kwa mwezi. hili litakuwa bunge la ufisadi,

    ReplyDelete
  3. Nilikuwa nawaambia watu kwamba huyu mwanamke mnayemwita makinda sidhani hata kama hao makinda anao, vinginevyo angekuwa na huruma kwa watoto wa wanawake wenzie. sasa nadhani wenyewe mnaona mtu anatumwa na wananchi aende kuwatetea yeye anaenda kutetea psosho huku akisistiza wanafunzi wanaodai poshzao ili wasome vizuri wafukuzwe mi sijui tumetokana wapi na huyu mwanamke yaani ananiudhi natamani hata asiwepo kabisaaaa! I real hate u makinda. Unathubutu kusema wabunge wamekuwa ombaomba ina maana hao ombaomba hapo dodoma na ni nani wa kupaswa kusaidiwa kwa kupewa posho unayoitetea? Wewe ni mwanamke ulithubutu kutoa hoja kwamba posho za wabunge zipo kisheria kwahiyo hazifai kuondolowa wala kubadili sera zake, na wakati upo bungeni unaongoza chombo cha kutunga na kurekebisha sheria. Huoni kuwa sasa zile fikra za kuwapumbaza na kuwadaa watanzania kwa maneno ya "amani na utulivu". Tumechoka na hii serikali naomba mtambue hilo na mimi binafsi nikipata utaalamu wa kutengeneza mabomu au nikipewa bomu nipo tayari kujilipua na mmoja wa ninyi mnaojiita viongozi wa mhimili ya taifa kumbe n wezi wakubwa na hakika nitafanya hivyo. Kwangu mimi sasa kuishi na kufa yote sawa....nimemaliza chuo kikuu nina miaka mitatu mtaani ajira hakuna fursa zote ni kwaajili ya watoto wenu sasa naishi ili iweje? Mnatutishia kwa mabomu na bunduki za polisi basi endeleeni hivyo maana tukifa sisi ninyi mtaishi milele. Naandika kwa uchungu sana, mnafanya mambo hata MUNGU hamumwogopi mnadhani dunia ni yenu.

    ReplyDelete