Na Mwali Ibrahim
TIMU za Simba na Yanga, zinatarajia kuchagia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.Simba na Yanga
zitachangia fedha hizo, kutokana na mapato yatakayopatikana katika mechi za kirafiki zitakazocheza na timu ya Escom ya Malawi.
MICHEZO ya kirafiki ya timu za Yanga na Simba dhidi ya timu ya Escom United Malawi inatarajia kutumika kuchangia waathirika wa mafuriko ya mvua yaliyotokea maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.
Mechi hizo ambazo zilikuwa zichezwe kesho na keshokutwa jijini Dar es Salaam, sasa zitapigwa Desemba 26 na 27, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na mratibu wa mechi hizo, Salum Mkeni ilieleza katika kila tiketi itakayokatwa sh. 500 itachangia waathirika hao.
"Tumesikitishwa sana na janga kubwa kama hili, kwa kuwa hakuna mtu alitegemea mafuriko haya kwani watu wengi wamepoteza maisha, tumeamua kuongeza sh. 500 katika mechi hizi kuwasaidia walioathirika," alisema.
Mkemi ameziomba kampuni mbalimbali kudhamini mechi hizo ili kufanikisha kupatikana kwa fedha za kuwasaidia watu hao.
No comments:
Post a Comment