29 December 2011

Rihanna amwigiza Michael Jackson

LONDON, Uingereza

RIHANNA ametayarisha video ya wimbo wake mpya, ambayo anaonekana akiwa amevaa mavazi yanayobana mwili huku akicheza kwa kuigiza mitindo ya
aliyokuwa mfalme wa pop, Michael Jackson.

Katika video hiyo ya wimbo wa You Da One, anaonekana akigusa sehemu zake za mbeleni karibu mara 20.

Kwa mujibu wa wa The Sun, video hiyo na uchezaji wake ni wa kusisimua zaidi kuliko Jackson.

Katika kuutangaza wimbo wa We Found Love looked, alionekana kung'ara zaidi.

Katika wimbo wake mpya, amepigwa picha Mashariki mwa London na inaonekana katika mtindo wa picha nyeupe kwa nyeusi.

Mwanamuziki huyo wakati wa Krismasi, alirejea kwao Barbados baada ya kutumbuiza katika Uwanja wa O2 Arena mjini London.

Hivi karibuni alilitunukiwa tuzo ya mwaka 2011 ya Mwanamke Mwenye Vituko.

Katika sherehe za Krismasi, alijichanganya na marafiki lakini hakunywa kiasi kingi cha pombe.

Chanzo kimesema kuwa alikwenda kwenye mgahawa na kununua vyakula vya habarini (samaki) na kula na rafiki zake.

Kisha alikwenda mlimani, ambapo watu hukusanyika na kucheza muziki.

"Alipendeza mno. Alipanda juu ya gari la Jeep na kuanza kucheza na kuwavutia watazamaji."

No comments:

Post a Comment