29 December 2011

Nelly ashika nafasi ya 5 China

Na Mwali Ibrahim

MREMBO Nelly Kamwelu, ameshika nafasi ya tano katika mashindano ya Dunia 'Miss Tourism Queens Internation' yaliyofanyika juzi nchini China akiwa mshiriki pekee
kutoka Afrika.

Nafasi ya kwanza katika mashindano hayo ilichukuliwa na mrembo kutoka Thailand, Kantapat Peerada huku nafasi ya pili ikinyakuliwa na Jeanine Castro wa kisiwa cha Fernando de Norontia.

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Maria Ovechkina kutoka Belarus huku nafasi ya nne ikienda kwa Mchina, Wang lu.

Mashindano hayo yalishirikisha warembo 92 kutoka Duniani kote, ambapo Namibia mshiriki wake alifanikiwa kuingia 10 bora huku mrembo wa Afrika Kusini akiishia nafasi ya 20 bora.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na mratibu wa mashindano hayo nchini kutoka Kampuni ya Compass Communication Limited, Maria Sarungi ilieleza, kuwa wamefurahishwa na Nelly ambaye ni Mtanzania wa kwanza kushika nafasi hiyo..

"Nelly ameweza kutuwakilisha vyema, tangu tuanze kushiriki na tumefurahishwa sana na nafasi hiyo na tutarudi nchini kesho kutwa (kesho)," alisema Maria.

No comments:

Post a Comment