Na Rachel Balama
MARAIS nane kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), na Makamu wa Rais wa tatu, wamethibitisha
kuhudhuria kilele cha maadhimisho yNa Rachel Balama
MARAIS nane kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), na Makamu wa Rais wa tatu, wamethibitisha kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 9 mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari na Waziri Mkuu Bw.
Mizengo Pinda, ilisema maadhimisho hayo yatafanyika katika Uwanja wa Uhuru ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.
Alisema alitoa mialiko kwa viongozi hao
ili kujumuika na Watanzania kusherehekea
miaka 50 ya uhuru ambapo mbali ya viongozi
hao, pia kutakuwa na makamu watatu wa Rais
pamoja na wawakilishi 16.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa, Rais Kikwete
pia ametoa mialiko kwa viongozi wa kitaifa
waliopo madarakani, wastaafu na vyama vya
siasa kwa Wenyeviti na Makatibu Wakuu.
Alisema mialiko maalumu imetolewa kwa wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa, wazee mashuhuri kutoka mikoa mbalimbali, baadhi ya Wenyeviti na Makatibu wa chama tawala.
Akizungumzia mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2011, Bw. Pinda alisema zimetumika kama sehemu ya maadhimisho hayo kuelezea mafanikio ya Serikali baada ya kuwashwa na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kijiji cha Butiama, mkoani Mara.
Alisema ujumbe wa mbio za Mwenge wa uhuru mwaka huu unasema “Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi Kusonga Mbele” na kusisitiza kuwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI, dawa za kulevya na rushwa pia ni sehemu ya ujumbe huo.
Mkesha wa maadhimisho hayo utakuwa Desemba 8 mwaka huu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.Pamoja na shughuli mbalimbali zitakazofanyika siku hiyo, pia kutakuwa na gwaride ambalo limeandaliwa na Vikosi ya Ulinzi na Usalama pamoja na onesho la zana mbalimbali za kivita.
Alisema pia kumeandaliwa halaiki maalumu ya wanafunzi wa shule
za msingi 4,550 na wanafunzi wa shule za sekondari na wahamasishaji
2,000. Sherehe hizo pia zitapambwa na ngoma za asili.
a miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara, Desemba 9 mwaka huu.

Ha ha ha ha Eti miaka 50 ya uhuru.
ReplyDeletetuna kila sababu ya kujivuania uhuru wetu kwani miaka ya 50 nchi ikiwa na amani si kitu cha kubeza hatuana vyote ila amani ipo hongera tz
ReplyDelete