02 December 2011

KATIBA MPYA:

CUF kuteta na JK Ikulu leo

Na Mwandishi Wetu

KAMATI Maalumu ya Chama cha Wananchi (CUF), leo inatarajia kukutana na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam, ili
kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zilieleza kuwa, kiini cha mazungumzo hayo ni kutokana na ombi la chama hicho kutaka kuzungumza na Rais Kikwete ili kutoa maoni yao kwa lengo la kuuboresha mchakato mbali ya kusainiwa.

CUF iliwasilisha serikalini rasimu yake ya Katiba Mpya tangu Desemba 28,2010 na kuitaka serikali ihakikishe inafanyia kazi mawazo hayo kwa masilahi ya Taifa.

Chama hicho kilikuwa cha kwanza kudai Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi mwaka 2000 baada ya kudai kuwa, Katiba ya sasa ni kandamizi ndiyo maana walishindwa kupata madaraka ya kuongoza.

Kutokana na hali hiyo, CUF iliitisha maandamano mbalimbali nchini ili kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Viongozi watakahudhuria mazungumzo hayo Ikulu leo ni Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa, Bw. Machano Hamis Ali, Bw. Julius Mtatiro, Naibu Katibu Mkuu Bara, Bw. Ismael Jusaladhu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Wengine ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi, Bw. Abdul Kambaya, Wabunge wawili, Bw. Habib Mnyaa na Bi. Mkiwa Kimwanga pamoja na Mwanasheria wa chama hicho, Bw. Twaha Taslima.

4 comments:

  1. du sasa CUF nini tena CCM iwafanyie kwa sababu awali mmejifanya watu wema na kuungana na chama tawala hali ninyi ni wapinzani halafu mmeona CHADEMA imelonga na Kikwete eti nanyi mwa safisha nyota ya chama kwa kuzulu ikulu Hampati kitu.

    ReplyDelete
  2. Dunia hii ina wehu wengi kweli,tuna misukule ya chadema nchini. kuna tatizo gani CUF kuonana na JK. fursa imetolewa kwa kila mmoja.Nyie wachaga hizo pesa za wafadhili zitaimaliza nchi.

    ReplyDelete
  3. Enyi CUF mtambue kuwa mnabeba jukumu la wazanzibari na haki zao , mkishindwa kututetea na haki zetu mjue kuwa mbele ya Mola mtawajibika na hamtapata msamaha wowote kwake. Tunataka katiba tatu ya znz( tutajua sisi nini tunataka), ya bara ( watajua wenyewe nini wanataka ) na ya muungano ambayo itachangiwa na wote wa bara na waznz. Tumechoka kutawaliwa na watanganyika , tunaomba mtupe uhuru wetu tuendeleza visiwa vyetu wenyewe. Tushirikiane kwenye mambo tutayokubaliana ktk muungano mpya , muungano wa Nd Nyerere and Nd Karume ulikuwa baina ya msomi na mbumbumbu.

    ReplyDelete
  4. ...another publicty stunt from bankupt CUF politicians...

    ReplyDelete