TIMU ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), leo itashuka uwanjani kucheza na Malawi saa 8 mchana katika
robo fainali ya michuano ya Tusker Chalenji, itakayochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kili Stars ilipenya hatua hiyo kutokana na kuwa na uwiano mzuri katika Kundi C, ambapo ilifungwa mechi mbili na kushinda moja.
Mechi hii ya leo kwa Kili Stars, ni muhimu kwao kushinda kama kweli inataka kutetea ubingwa wake iliyounyakua mwaka jana.
Katika hatua ya makundi timu hiyo haikuweza kufanya vizuri, kitu kilichosababisha mashabiki wa soka nchini kuiponda kutokana na kiwango chake.
Hivyo leo timu hiyo inatakuwa kushinda kwa udi na uvumba, ili iweze kufufua matumaini kwa mashabiki.
Hata hivyo Kocha Mkuu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa alisema licha ya kwamba kuna baadhi ya mashabiki hawawaungi mkono, watahakikisha wanashinda katika mechi zilizopo mbele yao.
Katika hatua ya makundi, hiyo ilianza kwa kufungwa bao 1-0 na Rwanda, ikaifunga Djibouti mabao 3-0 na ikafungwa na tena na Zimbabwe mabao 2-1.
Viingilio katika mechi ya leo vitakuwa sh. 2,000 na sh. 5,000. 10,000 na sh. 15,000 tofauti na viingilio vya awali ambavyo vilikuwa sh. 1,000 na sh. 10,000.
Mechi nyingine itakayopigwa saa 10 jioni itazikutanisha Burundi na Zimbabwe.
No comments:
Post a Comment