02 December 2011

Kesi ya Liyumba kuendelea leo

Na Rehema Mohamed

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, leo inatarajiwa kuendelea kusikiliza kesi ya kukutwa na simu gerezani inayomkabili
aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw.Amatus Liyumba.

Kesi hiyo ambayo inasikilizwa na Hakimu Stuwart Sanga, itakuja mahakamani hapo kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Katika kesi hiyo Bw.Liyumba anadaiwa kukutwa na simu akiwa gerezani Ukonga, Dar es Salaam, wakati akitumikia kifungo cha miaka miwili, kilichotokana na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi.

Inadaiwa kuwa, Julai 27, mwaka huu, katika Gereza la Ukonga, mshtakiwa alikutwa akiwa na simu gerezani kinyume na kifungu namba 86, kifungu kidogo cha kwanza na pili cha Sheria ya Magereza iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Katika kesi hiyo Bw. Liyumba yuko nje kwa dhamana ambapo upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

No comments:

Post a Comment