* Mahakama yasema hakuna ushaidi kumtia hatiani
*Yeye asisitiza moto ni ule ule, hakuna kurudi nyuma
Rehema Maigala na Aisha Muya
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jana, imewaachia huru aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) Bw. Jerry Muro, na wenzake waliokuwa wakikabiliwa na shitaka la kuomba rushwa ya Sh. milioni 10 kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha shitaka dhidi yao.
Washitakiwa katika kesi hiyo walikuwa wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwepo la kumuomba rushwa ya Sh milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Bw.Michael Wage.
Akisoma hukumu hiyo mahakamani hapo jana, Hakimu Bw. Frank Moshi, alisema kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa anawaachia huru na kuongeza kwamba rufaa iko wazi.
Katika hukumu hiyo Hakimu aliongeza kuwa vidhibiti vilivyofikishwa mbele ya mahakama hiyo na upande wa mashitaka vilikuwa haviendani na kesi hiyo.
Alisema pingu, bastola na risiti yake na miwani vya mshitakiwa wa kwanza havikutosheleza kuonyesha ni jinsi gani vilishiriki katika kesi hiyo hivyo ameamuru mshitakiwa kurudishiwa.
Hakimu Moshi wakati huyo akisoma hukumu hiyo alimshangaa Bw. Wage ambaye alikuwa mmoja wa shihidi wa upande wa mashitaka kushindwa kutumia nafasi yake akiwa kama kiongozi wa serikali wa kuwaomba wathumiwa wa kesi hiyo vitambulisho kama walijitambulisha kuwa ni maofisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Washitakiwa Bw. Jerry Muro, Edmund Kapama na Deogratius Mugasa kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani Februari 5 mwaka jana wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama kuomba rushwa ya sh. milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya bagamoyo, Bw. Michael Wage.
Wakati wa usikilizaji wa shauri hilo upande wa mashitaka uliwasilisha mashahidi saba na vielelezo.
Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Januari 28 mwaka jana Jijini Dar es Salaam walikula njama ya kutenda kosa la kuomba rushwa.
Shitaka la pili ilidaiwa kuwa, Januari 29 mwaka jana katika Hoteli ya Sea Cliff Dar es Salaam waliomba rushwa ya Sh. milioni 10 kutoka kwa Wage.
Ilidaiwa kuwa washitakiwa hao waliomba rushwa kwa lengo la kuzuia kutangazwa kwenye televisheni habari za tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zinazomhusu Bw. Wage akiwa mhasibu wa halmashauri hiyo.
Bw. Muro alikamatwa Januari 31 mwaka jana baada kwa tuhuma hizo na kushikiliwa kwa saa saba Kituo Kikuu cha Polisi Dar es salaam na kuachiwa baadaye.
Watuhumiwa hoa walifikishwa mahamani hapo na kusomewa mashitaka yao na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali, Bw. Boniface Stanslaus, akisaidiana na mwendesha mashitaka kutoka TAKUKURU Bw. Ben Lincolin, mbele ya Hakimu Mkazi, Bw. Gabriel Mirumbe.
Washitakiwa hao baadaye waliachiwa kwa dhamana ya kusaini hati ya dhamana ya Sh. milioni tano kila mmoja na kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika hivyo kuendelea kufika mahakamani wakati kesi ikiendelea.
Juni mwaka jana, upelelezi wa kesi hiyo ulikamilika na upande wa mashitaka ulidai kuwa utakuwa na mashahidi 11 huku Bw. Wage akiwa mmoja wa mashahidi hao.
Kwa upande wake Bw. Muro licha ya kuishukuru mahakama hiyo kutenda haki pia aliwashukuru watanzania wote wenye mapenzi mema na taaluma ya habari wakiwemo viongozi wa dini waliomwombea kuhisnda kesi hiyo.
Alisema kesi hiyo imekuwa ni chachu ya kufanya kazi yake ya uandishi wa habari kwa nguvu zaidi na kuweka wazi kuwa taaluma hiyo ni wito hivyo kuahidi kuendeleza vita dhidi ya vitendi viovu katika jamii na kamwe hataogopeshwa na hali hiyo na kurudi nyuma.
Alisema anawasamehe viongozi wote wa serikali walioshiriki kwa namna moja au nyingine kumkandamiza katika kesi hiyo huku wakijua kuwa alikuwa hausiki kwa namna moja au nyingine.
Hata hivyo upande wa Jamhuri uliweka wazi kutokubaliana na huku hiyo na kuanza taratibu za kukata rufaa.

Jamuhuri haina wataalam wazuri wa mashtaka! Au sijui uhaba wa vifaa na vitendea kazi, Huu ni muendelezo wa maovu kama ya Zombe, Jamuhuri inakosa kuwasilisha vitu muhimu! Hivi walishindwa vipi kupta print out ya mazungumzo yao ya simu? kampuni za simu zinamaana gani kama zitashindwa kutoa doc hiyo muhimu ikitakiwa na jamuhuri kufanya hivyo? hakuna tofauti kati ya kesi hii na ya Zombe, Chenge, Lowasa, Balali, Luhanjo na sasa Muro! mwisho wanabaki kutamba tu
ReplyDeletehii kesi ilitengenezwa na aliekuwa waziri kipindi hicho marsha, sasa hili serikali ionekane inafanya kazi lazima wakate rufaa, lakini hayo yoye ni danganya toto tu, watanzania tumeamka sasa,
ReplyDelete