27 December 2011

Jairo hana kosa, ni majungutupu-Mchungaji

Na Anneth Kagenda

MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC) lililopo Ubungo Dar es Saama, Mchungaji Antoni Lusekelo, ameibuka na kusema kuwa sakata la Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo, na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo, ni majungu na haina tatizo.

Bw. Jairo anadaiwa kuchangisha fedha za umma kwa ajili ya kugharamikia kupitisha bajeti ya wizara hiyo kinyume cha utaratibu huku Bw. Luhanjo akidaiwa kumjingia kifua.

Mchungaji Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako amesisitiza kuwa wapo viongozi wengi waliofanya kitendo sawa na ya Bw. Jairo lakini hayajulikani hivyo kutaka Watanzania kuacha tabia ya kuchafuana.

Akizungunza na waandishi wa habari Kanisani kwake jana, Mchungaji Lusekelo alisema haiwezekani mtu mmoja kupanga kuchangisha fedha za wizara bila kuwa na mtandao na viongozi wengine na kudai kuwa kilichotokea ni siri kuvuja na si vinginevyo.

"Ninachojua ni kwamba wezi wote wako mahakamani, unapoona mtu analalamikiwa kila siku wala hakamatwi ujue ni majungu tu na mambo hayo hafanyi, angefanya angekuwa selo

Ikumbukwe kwamba kuharibiana na kuchafuana kupo, mfano mimi niliwahi kuambiwa kwamba nimeenda nchini Nigeria kutafuta nguvu za giza wakati sijawai hata kuwaza kufanya kitendo cha namna hiyo,"alisema Mchungaji Lusekelo.

Aliendelea "Lazima tukiri kwamba watu wanachafuana na ndio maana ninasema hata kwa Bw. Jairo ni siri tu ilivuja na hawezi kufanya peke yake," alisisitiza.

Kuhusu maadili ya uongozi alisema anasikitishwa na kutoweka kwa desturi ya viongozi wa zamani ambao walilala na kuamka wakiwa na mawazo ya nini kifanyike tofauti na ilivyo sasa.

"Nchi imekuwa Imara, Amani na utulivu kutokana na watu fulani viongozi wa kwanza walikuwa wakiwaza na kujua kwamba kesho waamke na lipi lakini maisha ya sasa yanachangamoto nyingi na hii inatokana na uhuru wa utandawazi ambao unakuwa zaidi

"Lakini pia utandawazi huu usisababishe viongozi kujisahau na kudhani kwamba mwisho wa dunia ni 2015, bado kuna miaka mingine mingi na pia mawaziri na wabunge wasipende kujilimbikizia mali na kuwasahau wananchi wake," alisema Mchungaji Lusekelo.

Akizungumzia janga la mafuriko ya hivi karibuni alisema viongozi ndio watuhumiwa wa kwanza na kwamba wakati wananchi wanajenga mabondeni wanawaona na kuwanyamazia.

"Mvua ilikuwa ya kawaida sana ila tatizo ni watu kujenga sehemu ambazo siyo stahiri na huu ni uzembe wa watu.

Pia watu wanaambiwa wahame nao wanakaidi amri zinazotolewa na kusema kuwa hawaondoki mabondeni na wanataka walipwe fidia, fedha zitatoka wapi,"alihoji.

Aliwashangaa watu wanaobeza mafanikio ya miaka 50 ya Uhuru wa nchi na kusisitiza kuwa wengi wa wanaobeza maendeleo ya nchi ni vijana lakini ukweli ni kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa kwa kipindi hicho.

Kuhusu vurugu ya kisiasa, alisema migogoro ya kisiasa ilikuwepo hata kabla ya miaka 50 ya uhuru na kwamba siyo mipya hivyo kuwataka viongozi kufanya kila liwezekanalo kukabiliana nayo.

Aliwataka wanasiasa na kila mtanzania kumshukuru Mungu kwa ajili ya amani ya nchi na kuweka wazi kuwa kila mzalendo anapaswa kuwa adui na anayechezea amani ya nchi.

Tayari Bunge imetoa azimio la kuitaka serikali kumchukulia hatua za kinidhamu Bw. Jairo na Bw. luhanjo.

Hata hivyo baadhi ya wanasheria waliwai kuiambia gazeti hili kuwa kuna uwezekano mdogo kwa watendaji hao wa serikali kuchukuliwa hatua kama ilivyoamriwa na bunge.


17 comments:

  1. why is hawa wachungaji always seems to meddle in politics. Let them preach in their church the word of God and leave politics alone

    ReplyDelete
  2. Lo!!!!!!!!! Namshangaa mzee wa upako kutetea mafisani au na wewe uko kwenye system??? Fundisha watu wa Mungu Injili iliyo hai.Au La!! hamia kwenye siasa tujue moja.

    ReplyDelete
  3. Alichokifanya Jairo kinafanyika katika wizara zote, ikifika kipindi cha bajeti wanatakiwa kuchangia kiasi fulani ili kusaidia kupitisha bajeti. Kamati ya bunge ilitakiwa kuangalia wizara zote.

    ReplyDelete
  4. Hata kama tatizo liko kila Wizara Jailo kakamatwa hivyo lazima ashughurikiwe iwe fundisho kwa wengine huwezi kumtetea kwa maneno yasiyo na hoja kama haya ya mtu aliye jipa uchungaji.

    ReplyDelete
  5. Siamini kwamba ni Mzee wa upako anayesema kuwa eti Jairo amefanyiwa majungu kwa sababu uhalifu huu hufanywa na wizara zote na kwamba asingefanya peke yake.
    Lusekelo kwamba kama watu wanatenda dhambi wako wengi kunahalalisha kuwa aliyedhihirika wazi hana dhambi. Labda iwe umenakiliwa vibaya lakini kama ndivyo ulivyosema tunaanza kupata shaka kwamba sasa wenye dhambi wameamua kutumia kanisa kujisafisha na watumishi wa Mungu wamekubali kutumika kuwasafisha mafisadi.
    Hatukatai kama wamekiri na kutubu makosa yao basi jamii iambiwe ili tuendelee kuwachunguza kama kweli toba yao ilikuwa ya kweli.

    ReplyDelete
  6. Kosa ni kosa hata kama wengine wanafanya, hili liwe ni fundisho kwa viongozi wa umma hata wa dini kuwa mnapotumia vibaya madaraka yenu kufuja fedha za wananchi na waumini ipo siku siri itafichuka na yatawapata kama ya Jairo.

    ReplyDelete
  7. Nadhani suala la Mhe. Jairo ni kweli ni majungu na chuki binafsi kati yake na Mhe. Mbunge aliyeibua jambo hilo.

    Mbunge aliyeibua anaonekana hana hoja za msingi wa kumchafua Mhe. Jairo.

    Chunguzeni kiundani, mtapata ukweli.

    Mbunge kama huyu ni hatari kwa jamii.

    ReplyDelete
  8. Au wanaoibua chuki kwa David Jairo ni wanalipwa na maadui wa Jairo au Serikali yetu?

    Mhe. Raisi, sisi wananchi tunakupenda sana. Ni wachache sana tena wenye sauti ndio wanaokuvurugia mipango yako mizuri kwa jamii yetu.

    Jairo hana kosa. Ni mchapa kazi mzuri na mwaminifu kwa Umma. Barua inayotuhumiwa ni ya wazi na ya kikazi, haikuwa na siri au kuonyesha mazingira ya wizi. Benki pia sio ya binafsi.

    Mbunge Shelukindo hafai, ni mchonganishi. Anajua mwenyewe anachokifanya.

    Na wote wanaodanganywa naye naweonea huruma. Hawana hata maono?. Ni kama waliodanganywa na Babu wa Kikombe.

    Milango ya watu wa Mungu kama Jairo kamwe haifungwi na wachochezi kama shelukindo. Mungu atamfungulia tu Jairo na kuendelea kuwa Kioo cha Jamii. na wabaya wa maendeleo washindwe na walegee.

    ReplyDelete
  9. Nakubaliana na Mzee wa Upako. Tatizo sio Jairo bali mbio za kutaka uongozi na ulafi wa wanaomtuhumu Jairo.

    Wanajua kupitia tuhuma hizo, ndio wataweza kumng'oa Kikwete kwenye kiti cha Uraisi kabla ya muda wake kuisha.

    Hawapendi Kikwete atuletee maendeleo sisi Watanzania. Wanataka kuwe na misuko suko migomo, kuchafuana na maandamano, mikong'oto tu.

    Wananchi wote tunajua kuwa Jairo sio issue. Issue ni mbio za kuwania kuishika Ikulu.

    Nawakemeeni wavunjwa amani! Hamtashindaaaaaaaaaaa!

    ReplyDelete
  10. Nchi hii inakoelekea ni kubaya sana, yeyote anaweza kusema lolote japo halina msingi wowote. Wakati wa Nyerere kiongozi akionekana na tatizo hata kama ni rumours tu waliwajibishwa. Kama ni upole wa Rais wetu basi hii imekuwa tuu machi. Kama siyo upole basi there is something bad behind the president that has made him weak!

    ReplyDelete
  11. Hivi, nyinyi watu hamumwelewi mzee wa upako? Nataka nitumie mamneno yake mwenyewe "Ninachojua ni kwamba wezi wote wako mahakamani, unapoona mtu analalamikiwa kila siku wala hakamatwi ujue ni majungu tu na mambo hayo hafanyi, angefanya angekuwa selo" Aliongeza kuwa "alisema haiwezekani mtu mmoja kupanga kuchangisha fedha za wizara bila kuwa na mtandao na viongozi wengine" Hebu fikirini kwa undani maneno hayo.

    Pia soma maneno yake haya hapa "Lakini pia utandawazi huu usisababishe viongozi kujisahau na kudhani kwamba mwisho wa dunia ni 2015, bado kuna miaka mingine mingi na pia mawaziri na wabunge wasipende kujilimbikizia mali na kuwasahau wananchi wake".

    Ila napenda kukiri kwamba inahitaji kutuliza sana akili ili uweze kumwelewa Anthon Lusekelo, vinginevyo utajazwa na hasira kali.

    ReplyDelete
  12. Oya oya maneno mengi mtasema ila ukweli ni kwamba jairo na luhanjo wanafahamu walichofanya ni makosa,ila watu wanaolishwa na jairo na luhanjo plus wadau wao wa karibu wanafumbia macho ukweli. Km walichokifanya ni haki haiwezekani wabunge karibu wote, na hata wanachi makini wawanyooshee vidole bure. But pia km hilo ni haki basi vifungu vya sheria na mamlaka ya kufanya hivyo visingekosekana. Nikimsoma Anthony naelewa kuwa Jairo na luhanjo wananetwork na watu wenye maamuzi ya juu ndo maana serikali hawachukui hatua as if yale ni majungu tu. Ipo siku kila mwizi atalipa kwa style yake.

    ReplyDelete
  13. Hivi uovu ukifanywa na wengi hubadilika na kuwa tendo jema? Kama ndivyo huyu alijipachika uchungaji hana sababu ya kukemea dhambi kwani wengi watenda dhambi! Hivi wote wasiokuwa na kesi mahakamani ni watu wema? Mbona yeye ananeemeka kwa sadaka za masikini wajinga ambao ni uhalifu? Tumpeleke mahakamani ili tumwondolee majungu? Hata suala la yeye na Kakobe kuishi nigeria lina ukweli, walikwenda kufanya nini miaka ile? Hana upako wowote, haya ni matapeli ya kimataifa! Wajinga ndo waliwao!

    ReplyDelete
  14. 'COVER UP,' 'COVER UP' 'COVER UP.' HIVI HUU MTINDO WA UPANDE WA SERIKALI NA BUNGE KUFUNIKA SHUTUMA(COVER UPS) UTAISHA LINI? KAMATI MBALIMBALI ZINAPEWA MAJUKUMU NA KULIPWA LAKINI BAADA YA KUTOA TAARIFA ZINAISHIA KWENYE KABATI ZA WAHESHIMIWA. ZIKIPELEKWA MAHAKAMANI ZIATACHUKUA MIAKA HADI SISI WATANZANIA TUSAHAU AU HASIRA ZIPOE. HATUSAU KAMWE.

    NAOMBA WATANZANIA WENYE UZALENDO NA NCHI YAO PAMOJA NA VIONGOZI WETU WASOME KWENYE INTERNET KISA CHA KASHFA YA WATERGATE YA MERIKANI NA KUFUNIKWA KASHFA HIZO (COVER UPS) ZILIVYOMUUMBUA RAIS NIXON NA VIONGOZI WENZAKE.

    YA JAIRO NI COVER UP TUPU. COVER UP ZIKO NYINGI TU. WABUNGE FANYENI KAZI ZENU ZA KUSHUGHULIKIA HIZI 'COVER UPS' AU WANANCHI WALIOWACHAGUA WATAWAUMBUA. KWA NINI WATUHUMIWA WAONEWE HURUMA? WAPEWE HAKI NA HAKI NI KWA PANDE ZOTE- MTUHUMIWA NA MWENYE MALI ILIYOIBWA, YAANI (MWANANCHI)

    NAOMBA VYOMBO VYA HABARI VICHAPISHE MAKALA YA WATERGATE ILI WATANZANIA (VIONGOZI NA WANANCHI) TUJIFUNZE ILI TUJISAHIHISHE.

    ReplyDelete
  15. NAMWULIZA SWALI REV. ANTONI LUSEKELO: Ikiwa baadhi ya wasaidizi wako/watumishi wakifanya mbinu chafu na wakakuibia sadaka au suti zako na ukachunguza kwa kina na kuwapata; Je, utaenda jukwaani uwaambie waumini waliotoa sadaka zao kuwa waliokuletea taarifa hizo ni wapika majungu? Ya Jairo na wenzake yaachie sheria. Wewe fuata ya Mungu. Acha mwizi aitwe mwizi pale inapodhibitika. Hata kama hataadhibiwa ili mradi watu wamfahamu ili wajihadhari naye.

    ReplyDelete
  16. Cover up! Cover up! Mchango wa Anonymous wa Jan. 16 umenigusa sana. Nashauri watakao soma mawazo yake wajaribu kusambaza ujumbe huu baada ya kuutafakari kwa undani na kwa kina zaidi.

    Wasomaji wa gazeti la Majira na hasa waandishi wa habari na mabingwa wengine wa kisiasa na kitaaluma wanaweza kusaidia kuondoa hili tatizo la KUFUNIKA SHUTUMA (COVER UPS).

    BUNGE LINA JUKUMU LA KUFUATILIA HIZI COVER UPS. KAMA WANAJIKUSANYA PAMOJA KWA SABABU YA WINGI WAO KICHAMA KWENYE BUNGE,ITABIDI WANANCHI WAWAJIBISHE KWA KITENDO CHA KUSHIRIKIANA NA WASHUTUMIWA WA MAKOSA MBALI MBALI.

    IKIBIDI WAJIUZULU HATA KABLA YA MUDA WAO BUNGENI KWISHA. LA SIVYO WAWE "IMPEACHED" NA WANANCHI. Wabunge wanauwezo wa "kumimpeach" hata Rais. Kwa nini na wao wasitendewe hivyo na wananchi wanavyokwenda kinyume na matakwa ya kulinda mali za nchi?

    ReplyDelete
  17. hivi mtu akitoa maoni yake achalia mbali cheo chake/wasidha au huduma yake cha kuangalia maoni yalitolewa sasa watu mnaanza ohh siamini kama ni mzee wa upako toa hoja acheni kuchambua huduma yake mnaofanya hivyo mna mtindio wa akili. Toa solution kama kakosea wewe toa maoni yako ya kilichozungumzwa sio unatongezea mada wabongo bana!!

    ReplyDelete