Na Mwandishi Wetu
UONGOZI wa klabu ya Yanga umewataka wachezaji wa timu hiyo kuripoti kambini ifikapo Jumapili.Akizungumza Dar es Salaam jana
Ofisa Habari wa Yanga, Luis Sendeu, alisema wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambili ili kuanza mazoezi Novemba 28, mwaka huu.Na Mwandishi Wetu
UONGOZI wa klabu ya Yanga umewataka wachezaji wa timu hiyo kuripoti kambini ifikapo Jumapili.
Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa Yanga, Luis Sendeu, alisema wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambili ili kuanza mazoezi Novemba 28, mwaka huu.
Alisema wameamua kuwaita kujiunga na kambi mapema, ili kuweza kujiandaa vyema na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom inayotarajia kuanza Januari, mwakani.
Akizungumzia usajili wa wachezaji wapya, watakaoongeza nguvu katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo, Sendeu alisema bado wapo kwenye mikakati na kwamba, lolote linaweza kutokea kuanzia sasa.
"Cha msingi ni kwamba wachezaji wetu, ambao tunao hadi sasa wanatakiwa kuripoti kambini Jumapili na kuanza mazoezi Novemba 28, haya masuala mengine ya usajili bado klabu ipo kwenye mikakati, itakapokuwa tayari tutaongea," alisema Sendeu.
Alisema wamekuwa wakifanya mambo yao, bila papara na kwamba wanachama na mashabiki wao wategemee mambo mazuri, kutokwa kwa timu yao.
Yanga ambayo ilianza mzunguko wa kwanza kwa kusuasua imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ikiwa ya pili ikiwa na pointi 27 nyuma ya Simba yenye pointi 28.

No comments:
Post a Comment