Na Agnes Mwaijega
NAIBU Katibu Wizara ya Maji, Bw. Bashiri Mrindoko, amesema upo umuhimu mkubwa kwa serikali kuongeza uwekezaji katika sekta ya
maji nchini ili kukabiliana na changamoto zilizopo.
Bw. Mrindoko aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mafunzo ya simu moja yaliyoshirikisha Wahandisi wa maji ili kuboresha utendaji kazi wa sekta hiyo katika mikoa mbalimbali nchini.
Alisema sekta hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinachangia kukwamisha mpango wa serikali kuhakikisha kuwa, Watanzania wote wanapata maji salama.
“Matatizo yanayoikabili sekta hii ni changamoto ya kitaifa hivyo nguvu zaidi inahitajika, Serikali imeamua kutoa mafunzo haya ili kuongeza ufanisi na kuboresha huduma ya maji kwa wananchi,” alisema Bw. Mrindoko.
Aliongeza kuwa, kupitia mafunzo hayo yatawasaidia Wahandisi hao kuzijengea uwezo mamlaka za maji katika mikoa yote nchini na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Aliwataka wananchi kuacha kuharibu miundombinu pamoja na kujiunganishia maji kiholela na kuongeza kuwa, hali hiyo inasabababisha upotevu wa fedha nyingi za serikali.
No comments:
Post a Comment