Na John Gagarini, Kibaha
WADAU wa soka nchini wameliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuitumia michuano ya Chalenji kuchagua wachezaji wengine watakaounda kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars) ya baadaye.
Mmoja ya wadau wa soka mjini hapa, Fahim Lardhi alisema kutokana na Taifa Stars ya sasa kuonekana haina uwezo wa kufanya vizuri katika michuano mbalimbali ni vyema timu hiyo ikafanyiwa marekebisho makubwa.
Lardhi alisema Watanzania kwa kipindi kirefu, wamekuwa wakitamani kuona timu yao inafanya vizuri, lakini timu hiyo imekuwa ikiwaangusha kwa kufungwa mara kwa mara.
"Tunafurahi kuwa tumefuzu hatua ya makundi ya kuelekea fainali za Kombe la Dunia 2014, nchini Brazil baada ya kuitoa Chad lakini kiwango kilichooneshwa na wachezaji wa timu hiyo ni cha hali ya chini sana.
"Tunaitaka TFF na mashabiki wasitafute mchawi ila ni vyema kikosi hicho kikasukwa upya," alisema Lardhi.
No comments:
Post a Comment