Kamati Kuu CHADEMA yaota mbawa, sasa J.pili
Na Rehema Maigala
BARAZA la Vijana wa Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (BAVICHA) limesema lipo tayari kufa kwa kile wanachodai kwua ni kutetea haki ya mtanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu msimamo wao na hali ya kisiasa nchini, Naibu Katibu Mkuu wa BAVICHA Bi.Ester Daff, alisema anawataka vijana wa chama hicho wasiwe waoga kusikiliza kauli alizoita kuwa ni za vitisho hali aliyodai kusababisha taifa kuangamia.
"Vijana tukubali kufa kwa ajili ya watanzania wenzetu, mpaka hivi sasa hatujui hili taifa linaelekea wapi viongozi wa juu wamekuwa hawawasikilizi wananchi wake inavyotakiwa,"alidai Bi. Daff.
Alidai Watanzania wengi wanahitaji muswada wa Sheria ya Kuundwa Tume ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba Mpya usomwe bungeni kwa mara ya kwanza ili waweze kupata fursa ya kutoa maoni yao.
"Katiba ni jambo la muhimu unaweza kufananisha na roho ya binadamu hivyo kila mtanzania mwenye akili timamu anatakiwa kuchangia maoni yake,"alisema Bi.Daff.
Naye Mwenyekiti wa Baraza hilo Bw. John Heche, alisema baraza lake limejadili kwa kina mchakato wa uundwaji wa katiba mpya na kudai kubaini kuwa muswada uliosomwa bungeni juzi ni batili kwa kuwa ulipaswa kusomwa kwa mara ya kwanza ili kutoa fursa kwa wananchi kuujadili kwa maelezo kuwa ule wa awali ulikataliwa.
"Azimio katika kamati yetu tendaji ni kupinga mchakato huu kwa kuungoza wananchi kupaza sauti zao za kuupinga muswada kwa nguvu zote ikiwemo maandamano yasio na kikomo kwa nchi nzima,"alisema Bw.Heche.
Alisema katika kamati yao wamejadili kwa kina mfumo mzima wa mikopo unaoongozwa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kudai kuwa unapopigania na kuendeleza juhudi kubwa za kuwanyanyapaa watoto wa watu masikini.
Alidai kitendo cha wanafunzi zaidi ya 12,000 kunyimwa mikopo kwa kukosa vigezo vinavyotakiwa ni jambo aliloliita kuwa ni la kihuni kwa kuwa mpaka sasa bodi ya mikopo haina uwezo wa kubaini ni nani masikini na tajiri kweli.
Alisema kamati yao pia ilizungumzia na kulaani kukamatwa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliotiwa mbaroni baada ya kutokea vurugu wiki iliyopita.
Wakati BAVICHA wakitoa kauli hiyo tayari wabunge kadhaa wameonyesha wasiwasi wao kuhusu kauli kama hizi huku zikitafsiriwa kuwa ni kutaka kuwachochea watanzania kufanya vurugu.
Hata hivyo mjadala unaoendelea nchini sasa ni jinsi ya kupata sheria ya kuundwa kwa Tume itakayokusanya maoni ya wananchi jinsi wanavyotaka Katiba Mpya uwe. Mjadala kuhusu Katiba yenyewe utaanza baada ya hatu hii ya sasa.
Naye Godfreya Ismaely anaripoti kutoka Dodoma kuwa
Kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilichopangwa kufanyika leo kimehairishwa.
Katibu wa wabunge wa Chama hicho Bw. Jonh Mnyika, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma jana kuwa wamelazimika kukisogeza mbele kikao hicho kutokana na umuhimu wa taarifa zinazowasilishwa bungeni.
Alisema uamuzi huo sasa utawafanya wabunge hao kuandamana kwa pamoja siku ya Jumamosi asubuhi kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki kikao hicho.
Alisema uamuzi huo unatokana na kikao cha kambi ya upinzani ambacho walikifanya jana na kuona kuna haja ya kufanya hivyo ili kutoa nafasi ya kushiriki katika uwasilishaji huo.
"Uamuzi ambao tumefikia pamoja na hatua ambazo kesho ( leo) tulipaswa tuzichukue kupitia kikao cha kamati kuu ambacho tuliwaelezeni jana (juzi)kwamba siku ya Alhamisi tungefanya hivyo kulingana na msimamo wetu wa kutoshiriki katika mjadala wa Muswada wa wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mwaka 2011," alisema Bw. Mnyika
Alitaja sababu za kuhairisha kikao hicho kuwa kuwapa nafasi wabunge wao ambao ni miongoni mwa wajumbe katika kamati ambazo zinahusika katika uwasilishaji Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya sheria mbalimbali za Biashara wa mwaka 2011 na taarifa ya kamati ya Nishati na
Madini watashindwa kushiriki.
"Baada ya kuona kwamba kesho (leo) Alhamisi kutakuwa na shughuli muhimu za kitaifa tumeona tukifanya kikao cha kamati kuu kesho baadhi ya wabunge ambao nao ni miongoni mwa wajumbe katika kamati Kuu ya Chama watashindwa kuudhuria kwa kuwa nao ni muhimu baada ya uamuzi huo tumeona kwamba ni vyema tukasogeza kikao chetu hicho ili tuwape nafasi hadi
jumapili,"
Alisema wabunge hao wataondoka wote bila kujali ni mjumbe katika
kamati kuu na lazima ashiriki kwenye kikao hicho cha jumapili ili
kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya hatua zaidi.
Kwa upande wake mbunge wa Singida Mashariki, Bw. Tindu Lissu
akijibu hoja za wabunge wanaomtuhumu kutotambua Muungano alisema
kwamba CHADEMA kinatambua muungano ingawa katiba ya Zanzibar ndiyo
inayoukataa.
Mabadiliko yanakuja kwa watu wachache kujitolea muhanga. Support ipo tu!
ReplyDeleteIpo siku and i think ndo imeshafika... tunaikomboa nchi kutoka kwa wezi hawa. Very soon.
ReplyDelete