*Serikali yahadharisha wananchi
*Kenya wakamata Watanzania 10
*Nahodha akerwa kauli za fujo
Na Reuben Kagaruki
SERIKALI imesema Tanzania inakabiliwa na tishio kubwa la kushambuliwa na kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab hivyo kuwataka wananchi kuchukua tahadhari pindi wanapoona watu wanaowatilia mashaka.
Tahadhari hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Shamsa Vuia Nahodha, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Bw. Nahodha alisema vipo viashiria vya aina nne vinavyoongeza hofu ya kikundi hicho kuishambulia Tanzania ikiwemo baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa ni Watanzania kuhisiwa kushirikiana na kikundi hicho.
Alisema tayari vijana 10 wa Watanzania wanadaiwa kukamatwa na jeshi la Kenya katika mpaka wa nchi hiyo na Somalia.
"Wapo Watanzania waliokamatwa mpakani mwa Kenya na Somalia ikisemekana walikuwa wakienda kujiunga na kikundi hicho," alisema Bw. Nahodha na kuongeza kuwa mbali ya hao, wengine wanarubuniwa kwa ahadi ya kwenda kutafutiwa kazi nje, matokeo yake kujikuta wakipelekwa kwenye vikundi vya kigaidi.
Alitaja kiashiria kingine kuwa ni kutokea kwa mashambulizi nchini Kenya ambayo yanahusishwa na Al-Shabaab na kuwaomba wananchi kuwa makini na mtu au kundi lolote linalojidai kuwasafirisha nje ya nchi kwa lengo la kwenda kuwatafutia kazi.
"Kenya yametokea mashambulizi kama matatu. Kenya ni jirani na sisi," alisema na kutoa mfano kuwa mwaka 1998 lilipotokea shambulizi la kigaidi nchini lilienda sambamba na lile la Kenya.
Hata hivyo aliwatoa wasiwasi watanzania na wageni wanaotembelea nchi yetu kutokuwa na wasiwasi kwa kuwa vyombo vyote vya dola vimejiandaa vya kutsoha kukibiliana na tishio la mashambuzi hayo.
"Vyombo vya dola vitaendelea kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu wanaohusika na vitendo hivyo, na Tanzania itaendelea kushirikiana na taasisi zinazopambana na ugaidi duniani,"alisema.
Alitoa mwito kwa wananchi kutoa taarifa wanapoona watu wanaowatilia mashaka au wanapokuwa wakinunua vifaa vya milipuko, kupiga picha maeneo mbalimbali ya mji ikiwemo ofisi za kimataifa ili vyombo husika vifutilie nyendo zao.
Kwa upande wa madereva taksi na vyombo vingine vya usafiri, waliwataka wawe makini kufuatilia nyendo za wateja wao hasa wale wanaotaka kupelekwa ofisi za kibalozi na maeneo mengine nyeti na kupiga picha.
Wenye nyumba za wageni na mahoteli nao wametakiwa kuwa makini na wageni wao na kuhakikisha kila mgeni anaandika taarifa zake kikamilifu katika vitabu vya wageni na kunakili namba za hati za kusafiria na kutoa taarifa za siri kwa vyombo vya dola kwa wale wageni wa nje wasiotaka kujitambulisha kwa uwazi na wasiokuwa na hati za kusafiria.
Mjadala wa katiba mpya
Akizungumzia kauli zinazolenga kuashiria uvunjivu wa amani na utulivu nchini zinazotolewa na viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wanaharakati, Bw. Nahodha aliagiza wachukuliwe hatua haraka na kushangaa sababu za kutamba kwao.
Bw. Nahodha alionekana kushangazwa na Jeshi la Polisi kukaa kimya, bila kuwahoji wanaotoa kauli za kutishia uvunjifu wa amani katika mchakato wa muswada wa kuundwa kwa sheria ya kuunda Tume ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya upatikanji Katiba Mpya uliowasilishwa bungeni juzi mjini Dodoma.
"Nigekuwa mimi ningewauliza ni kwa nini wanataka kufanya hivyo," alisema na kusisitiza kuwa mtu anayetoa matamshi ya kufanya kitendo kinacholenga dhamira ya kuvunja amani ni kosa.
"Usisubiri mtu anayekutishia kwa rungu akugonge kichwa, si busara kusubiri ushahidi hadi ugongwe," alisema na kuwataka watendaji walio chini yake kutimiza wajibu wao kwa kuchukua hatua vinginevyo watawajibishwa.
Bw. Nahodha alitoa kauli hiyo huku wabunge wa CHADEMA na wale wa NCCR-Mageuzi wakiwa wamesusa kushiriki mjadala wa muswada wa Sheria ya Kuundwa kwa Tume ya Kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba kwa madai kuwa haukidhi vigezo.
Pia Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willbroad Slaa, hivi karibunu alinukuliwa akisema pindi ukipitishwa wataupinga na ikibidi watatumia maneno makali.
Wanaharaka kwa upande wao tayari wametoa msimamo wao mkali na kwenda mbali zaidi kwa kuweka wazi kuwa pindi muswada huo utakapopitsihwa na bunge la Tanzania wataingia barabarani kuupinga kwa maandamano yasiyokoma.
Sakata la Jiji la Arusha
Katika hatua nyingine Bw. Nahodha, alijibu kile kinachoonekana kama shinikizo kutoka kwa viongozi wa CHADEMA kutaka Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, (OCD) Zuberi Mwombeji, ahamishwe kwa madai kuwa hazingati haki na kuweka wazi kuwa hawezi kufanya kazi kwa kushinikizwa.
"Nikimuondoa nitakuwa nimeshinikizwa, waziri hatakiwi kutishwa, nikikubali siku nyingine watasema mfukuze IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi), wakimaliza hapo watasema nijifukuze mimi mwenyewe," alisema na kusisitiza kuwa viongozi wa chama hicho walitakiwa kumpelekea malalamiko ofisini kwake na si kutoa shinikizo hilo kupitia mkutano wa hadhara.
nahodha wacha mbinu za kizamani! mnataka tusahau kuhusu katiba na ufisadi eeh? Waapi sie na nyie mpaka muondoke! Tumewachoka! Hatutaki CCM tena! Na nyie rudini kwenu Unguja mkale mihogo mikavu! Shwaini!
ReplyDeletesema ww mwenye mbinu mpya usikilizwe
ReplyDeleteHuyu Mh. Nahodha amesoma mpaka darasa la ngapi?. Naona majibu yake kama mtu asiyesoma na mwenye sias za CCM za kizaani ambazo zimepitwa na wakati.
ReplyDeleteKuhusu Al-Shabab namuomba Mh. Nahodha wasituingize kwenye mambo yasiyotuhusu maana tunaambiwa ya Ngoswe tuwaachie Ngoswe wenyewe.
Pili, mfupa uliomshinda fisi kweli utauweza wewe Mh. Nahodha mwenye meno ya kubandika
Al-Shabab wanavamia Kenya kwa vile wanakisasi na wa Kenya wamezoea kuwanajisi dada ao na mama zao wakisomali waliokimbilia Kenya. Sisi watanzania hatuna ugomvi na AL-Shabab hivyo msituzingue
ReplyDeleteMh. Nahodha Funga domo lako na ubabaishaji wa CCM imewatawala hadi akilini!.... mutajiongeza lini? Watanzania fumbueni macho acha kukorota changamsha akili. Na huo ni mtazamo wako wewe kama Nahodha. Yetu sisi Watanzania tunataka tushirikishwe kwenye mchakato wa katiba iliyochakachuliwa vibaya kama mlivyo zoe serikali ya CCM.
ReplyDelete