Na Rehema Maigala
IMEFAHAMIKA kuwa uchumi wa Tanzania umeendelea kukua na kufikia asilimia 6.3 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2011.
Akizungumza na wahandishi wa habari ofisi ya Wizara ya fedha mjumbe wa Shirika la fedha Duniani (IMF)Bw.Peter Allum ambaye alikuwa jijini Dar es Salaam kuanzia Oktoba 26 mpaka Novemba 7 kwa ajili ya kufanya majadiliano ya awamu ya tatu ya mapito chini ya mpango wa msaada wa kisera.
'' Licha ya matatizo ya upungufu ya nishati ya umeme Tanzania bado imeonekana kuwa inakuwa kiuchumi ''.alisema Bw.Allum
Alisema kuwa mfumuko wa bei usiojumuisha chakula na nishati umeendelea kuwa tarakimu moja,wakati mfumukowa bei ya jumla umekaribia asilimia 17 mwaka hadi mwaka kulikochangiwa kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la Dunia.
Aidha alisema miaka ya hivi karibuni matumizi
ya Serikali kama sehemu ya pato la Taifa yameongezeka ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya huduma za kijamii katika ngazi ya Serikali za mtaa hususan katika sekta ya afya, elimu na sekta zingine za kijamii.
Hilo alisema ni sambamba na kuongezeka kwa uwekezaji katika barabara na miundombinu mingine.
Hata hivyo alisema matumizi ya kawaida yalizidi mapato ya ndani pamoja na misaada iliyopelekea kukua kwa nakisi ya bajeti na kuongezeka kwa deni la Taifa.
Vilevile alisema kuwa nakisi ya bajeti ya mwaka 2011/12 izidi kile kiwango kilichowekwa kwenye mpango wa awali cha asilimia 6 ya pato la Taifa ili kugharamia mpango mpango wa dharura wa nishati na kukidhi matumizi ya upanuzi wa huduma za jamii.
Aidha alisema matumizi kwenye miradi isiyo ya kipaumbele yatapunguzwa ili kuhakikisha nakisi ya bajeti inapungua kutoka kiwango cha mwaka uliopita na kuwa kiwango kinachokaribia asilimia 6.5 ya pato la Taifa hivyo upunguzaji huu wa bajeti utawezesha juhudi za kiserikali za kupunguza mfumuko wa bei.
Hivyo Serikali ina mpango wa dharura wa kuzalisha umeme umehusisha uwekezaji wa Serikali na sekta binafsi katika uzalishaji mpya wa nishati ya umeme unaozalishwa na majenereta ambapo uwekezaji wa awali umesaidia kupunguza mgao wa umeme nchini.
lakini imeoneka kuwa uchumi wa Tanzania umezidi kukua.
.
No comments:
Post a Comment