11 November 2011

Stars yatua Chad salama

Poulsen ataja watakaonza

Na Boniface Wambura, N'djamena

TIMU ya ya taifa (Taifa Stars) imewasili jana usiku mjini hapa tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia, dhidi ya Chad itakayochezwa kesho Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya.

Stars imefikia hoteli ya Santana na jana saa 10 jioni kwa saa za hapa ilfanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya. Leo mechi itaanza saa 10 kamili jioni ambayo kwa  Afrika Mashariki itakuwa ni 12 jioni.


Wachezaji wote wako katika hali nzuri isipokuwa beki Erasto Nyoni, ambaye jana asubuhi ameamka akiwa na malaria.

Kocha Jan Poulsen alikitaja kikosi kitakachoanza kuikabili Chad leo kuwa ni Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Juma Nyoso, Idrisa Rajab.

Wengine ni Shabani Nditi, Henry Joseph, Abdi Kassim, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa na Mbwana Samata.

Waamuzi watakaochezesha mechi hiyo wote mechi wanatoka Nigeria.

Mwamuzi wa kati atakuwa Bunmi Ogunkolade wakati wasaidizi ni Tunde Abidoye na Abel Baba. Kamishna wa mechi ni Hamid Haddadj kutoka Algeria.

Stars imekuja hapa na kikosi cha wachezaji 21, ambacho kitarejea Tanzania baada ya mechi kwa ndege ya Ethiopian Airlines kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia.

Timu itawasili Novemba 13 mwaka huu saa 7.25 mchana na kwenda moja kwa moja kambini.

No comments:

Post a Comment