Na Amina Athumani
UONGOZI wa Simba, umewatoa kwa mkopo wachezaji wake beki Salum Kanoni aliyepelekwa Moro United na kiungo Amri Kiemba
Polisi Dodoma.
Wachezaji hao wametolewa na klabu hiyo, ili kwenda kupandisha viwango vyao vya uchezaji katika timu hizo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Godfrey Nyange 'Kaburu', alisema nafasi za wachezaji hao zimezibwa na wachezaji wanne waliopandishwa kutoka timu ya vijana ya Simba.
Kaburu alisema mbali na wachezaji hao, pia mchezaji Mohamed Kijuso ambaye ameichezea Villa Squd kwa mkopo, wameamua kumuuza kwa timu ya Ruvu JKT.
Alisema Shija Mkina aliyepelekwa kwa mkopo Kagera Suger wamemrudisha, lakini ameomba kuvunja mkataba na Simba, ili awe huru jambo ambalo klabu hiyo imeridhia na sasa inamwandalia utaratibu.
Kiongozi huyo aliongeza kuwa mchezaji Meshack Abel, yeye ameamua kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Botswana, hivyo wanamwandalia mazingira ya kutimiza azima yake.
"Tumekubaliana na Abel kwenda kucheza nchini Botswana, hivi sasa tunamwandalia mazingira mazuri aweze kutimiza azima yake na tunamtakia kila la heri kwa kuwa soka ndiyo maisha yake," alisema.
Wachezaji wa timu ya vijana waliopandishwa ni Frank Sekule, Abdallah Seseme, Hassan Khatib, Edward Christopha pamoja na beki Dereck Walulya kutoka Uganda ambaye ameziba pengo la Jerry Santo.
Kaburu alisema klabu hiyo kwa haina mpango wa kusajili mchezaji, ambaye hajapitia ngazi za chini kwa kuwa kikosi chao cha vijana ndiyo kitakuwa dira ya soka la Simba, kwani wachezaji wake wana ubora zaidi.
No comments:
Post a Comment