Na Heri Shaaban
MICHUANO ya kuwania Kombe la Malembeka, yameanza kutimua vumbi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mvuti wilayani Ilala, Dar es Salaam.
Katika mechi ya ufunguzi, Sangara na Kiboga ziliumana ambapo Sangara iliichapa Kiboga mabao 3-2.
Mabao ya Sangara yalifungwa na Hamisi Siza mabao mawili na Ally Kikwanyu bao moja, wakati mabao ya Kiboga yalitumbukizwa wavuni na Mohamed Shaba na Sultan Nassoro.
Mashindano hayo yaliyoanza mwishoni mwa wiki, yatashikisha timu tisa za Kata Msongola, yakiwa na lengo la kuinua na kuendeleza vipaji vya wachezaji chipukizi.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Mratibu wa mashindano hayo, Ibrahim Mbuzi, alisema katika michuano hiyo, vijana wengi wanaweza kusajiliwa na timu mbalimbali wakati huu wa dirisha dogo la usajili.
Ibahimu aliziomba timu za kata hiyo zizingatie kanuni za mashindano hayo ili ziweze kutwaa pikipiki ambayo zawadi ya mshindi, pikipiki, kombe, cherehani na kibao cha kufyatulia matofali.
Alisema zawadi zitakazotolewa na diwani wa kata hiyo kwa washindi zitagharimu sh. milioni nne
No comments:
Post a Comment