Na Amina Athumani
WACHEZAJI kumi kati ya 28, walioitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), wamechujwa katika kikosi hicho wakiwemo
Gaudence Mwaikimba na John Bocco.
Kilimanjaro Stars inatarajia kushiriki michuano ya Tusker Chalenji, ambayo inatarajia kuanza leo jijini Dar es Salaam.
Kikosi hicho ambacho ndiyo mabingwa wa tetezi wa michuano hiyo, kinatarajiwa kushuka kesho, uwanjani kuvaana na Rwanda 'Amavubi' katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura aliwataja wachezaji wengine waliochwa Dar es Salaam jana kuwa ni kipa Deo Munishi, Paul Ngelema, Salum Telela, Jimmy Shogi na Mohamed Soud.
Wengine ni Hussein Javu, Daniel Reuben na Nizar Khalfan.
Wambura alisema wachezaji waliobaki katika kikosi hicho ni makipa Juma Kaseja na Shabani Kado.
Aliwataja mabeki kuwa ni Shomari Kapombe, Godfrey Taita, Juma Jabu, Ibrahim Mwaipopo, Juma Nyoso, Said Murad na Erasto Nyoni.
Wengine ni viungo Shabani Nditi, Nurdin Bakari, Haruna Moshi 'Boban' na Mwinyi Kazimoto.
Aliwataja washambuliaji kuwa ni Said Maulid, Mussa Hassan 'Mgosi', Mrisho Ngassa, Ramadhan Chombo, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata na Rashid Yusuf.
No comments:
Post a Comment