25 November 2011

Kashilila aichefua CHADEMA upya

 *Wamshangaa kauingilia mambo yao, kupotosha umma
*Wamtaka awataje wabunge wachanga wasiojua sheria
*Mnyika amshukia Makinda, asema alipuuza wabunge

Na Benjamin Masese

SIKU moja baada ya Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilila, kudai mazungumzo kati ya Rais Jakaya Kikwete na Kamati teule ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hayatabadili maamuzi yaliyopitishwa na Bunge, chama hicho kimeibuka na kusema kuwa, kiongozi huyo hana msaada wowote kwa bunge bali anaeneza sumu, chuki na kuchonganisha makundi ndani ya jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, ambaye pia ni Katibu wa wabunge CHADEMA, Bw. John Mnyika, alisema wameshangazwa na kitendo cha ofisi ya bunge kuwa mstari wa mbele kupotosha umma juu ya muswada wa mabadiliko ya katiba mpya 2011.Alisema juzi Dkt. Kashilila alitoa taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa, baadhi ya wabunge wa Bunge la Muungano ni wachanga na hawajui sheria ambazo walipaswa kuzitumia kujenga hoja.

“CHADEMA inamtaka Dkt. Kashilila awataje wabunge hawa kwa majina na kueleza kwa nini alishindwa kuwashauri mapema ili waweze kutimiza lengo la muswada huo kutosomwa bungeni kwa mara ya pili,” alisema.
Alisema kitendo cha kusema majadiliano kati ya Rais Kikwete na kamati teule ya chama hicho hayawezi kubadili maamuzi ya bunge ni kutaka kupotosha Watanzania na dhamira ya Kamati Kuu ya CHADEMA kutaka muafaka kwa njia ya majadiliano.

“Hili suala ni bichi, upo uwezekano wa kutolewa maamuzi makubwa yasiyotarajiwa, Dkt. Kashilila anapaswa kusoma ibara ya 62(1) na 62(3) ya katiba ya Tanzania.

Alisema Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda aliwapuuza wabunge waliojitokeza kuonesha jitihada za kupinga muswada huo usisomwe kwa mara ya pili lakini si kweli kwamba wabunge hawajui sheria.
Bw. Mnyika alisema alikusudia kutumia kanuni ya 86(3)(a) kupinga muswada usisomwe kwa mara ya pili lakini alipuuzwa hata alipotumia kanuni ya 55 (3)(b) ili kutoa hoja ya kuahirisha mjadala.
“Huyu Dkt. Kashilila ndiye hajui sheria, alishindwa kulisaidia Bunge na kumshauri Spika wake, umma uliona yaliyokuwa yakitendeka, hata kanuni ya 86 (3) (b) ilipotumika, wabunge walisimama ili kuunga mkono hoja lakini haikusikilizwa.

“Kimsingi suala la kupitisha muswada huu lilikuwa limepangwa, nawaomba wananchi mpuuze kauli za Dkt. Kashilila, jambo la msingi tupiganie haki yetu ya kushirikishwa katika mchakato wa kupata katiba ambayo itatuongoza miaka 50 ijayo,” alisema.

Aliongeza kuwa kama Dkt. Kashilila atashindwa kuwataja wabunge wasiofahamu sheria na kueleza sababu za kushindwa kumshauri spika, watakutana na kutafakari hatua za kuchukua.

16 comments:

  1. Hivi huyu Kasilila naye amekuwa mwanasiasa? Ama kweli nchi hii haina mwelekeo!

    ReplyDelete
  2. Wananchi wote tunao ipenda nchi yetu Tangnyika,Zanzibar na hatimaye Tanzania TUKOMAE,TUKAZEUZI,Kupambana na mafisadi(CCM). Wanataka kujitengenezea katiba mpya ya kendeleza kuihujumu nchi yetu.Nawaomba wanahakati,watalaam,na wasiasa wazalendo kama CHADEMA na NCCR MAGEUZI mtuongoze wananchi kupata haki ya kuweka mustakabali wa nchi yetu.

    ReplyDelete
  3. kashishilia ni dr wa elimu au ni kama wale waganga wa jadi, nilimuona anongea kwenye TV niliamua kuzima nisimuone wala kusikia, anasema eti wadau kama 50 walichangia,ujinga kabisa. Hivi swala la katiba linajadaliwa na watu 50, hata sheria ndogo ya kijiji ni zaidi ni nusu ya wananchi wote wa kijiji itakuwaje sheria Mama ya nchi,Mie nawasiwasi na uwezo wake hata kama ni dr kwenye karatasi na siyo IQ kwichwani.in short ni galasa.

    ReplyDelete
  4. Mh.Dr.Kashilila,ninaomba asamehewe ni Mshamba wa Siasa.Masuala ya Mh.Rais yanamhusu nini?.
    Istoshe Dr.Kashilila hajui Job Discription zake,ninaomba amfundishe vizuri.

    ReplyDelete
  5. Niajabu kuona Dr Kafulila anao mchango wa namna gani. Ni wakimaslahi potofu! Wale wote wanaowalaumu Chadema eti bora wangebaki ndani ya Bunge wamepata uthibitisho tosha kuwa, Makinda na jopo lake, wangewaburuza na kupata uhalali hadi kupata uhalali wa kikebehi.Baada ya miaka 50 nchi imedorora kwa uzembe wa Katiba iliyowekwa na watu wachache ambao walishindwa kuona mbali kwa maslahi ya vizazi vyote. Walijiona wao wenyewe! Sasa najaribu kujiuliza upya!Hivi Marehemu Baba wa Taifa hakuliona hili la Katiba aliyoiacha isiyoruhusu kuhoji mshindi wa Urahisi aliyekwapua Kura na kutangazwahadi mshindi kitapelihata baada ya miak 25 akatuachia zengwe hili! Watanzania tukazane kutafuta haki zetu kwa moyo mmoja bila kukata tamaa tukiongozwa na vyama makini vyenye muono makini kama Chadema, NGOs, na wote walioko katika nyadhifa mbali mbali, hata ndani ya Serikali na CCM yenyewe. Kwa maana haiwezkani wanaccm wote mioyo yao haini hata chembe za uzalendo kidogo wa kuona jinsi Katiba hii mbovu inatufilisi: kifikra, kifisadi, kitaifa n.k.

    ReplyDelete
  6. Ukweli siku zote huwa unauma, tupeni sababu zxa Msingi zinazopelekea kutaka Muswada usisainiwe.
    Kila siku hamtoi sababu mmekuwa kama Bendara inayofuata Upepo: Mnyika anasema wapewe haki ya Msingi ya Kushirikishwa kwenye Mchakato wa Kupata katiba Mpya. Je ni hilo lililopelekea Chadema Mkatoka Bungeni? Watanzania hebu oneni haya!! Sasa hawa kweli wana uchungu na nchi hii, au ni Ubishi usiokuwa na tija. Ninavyofahamu mimi Watanzania wote tutapata fursa ya kutoa na kutaka katiba yetu iweje mbele ya Kamati teule Bila kificho na Bila Shuruti. Sasa hawa wanataka washirikishwe kwenye hiyo Kamati teule au wapi?
    Watanzania Tazameni na Mtafakari kwa Makini hawa wanataka kutupeleka wapi?

    ReplyDelete
  7. Ninvyofahamu mimi binafsi ni kwamba,dr.Kashilila ni katibu wa bunge lakini pia ni kama kibaraka wa ccm kwani bunge lenye asilimia kubwa ya wbunge wa chama kimoja katika ubunge huwa tunasema kwa tanzania ndio linaloongoza bunge kwani huwa wanatumia wingi wao ili kupata na kupisha kile wana chokitaka.

    Kashilila sioni kama amesema la kwake inawezekana katumwa na mtu au kiongozi wake spika,na mbaya zaidi kwa hayo aliyoyasema ikitokea rais akafanya tofauti na anavyosema itakuwaje?

    AACHE UJINGA NA HUO U-DR.WAKE

    ReplyDelete
  8. Jamani sisi sio watoto wa kudanganywa na kashilila, kwanza huyu kashilila lazima atetea wanaccm wenzie kwa sababu alifuja pesa za bunge lakini hakuna kilicho endelea. Kipindi hicho CCM kama kawaida yao wanafanya mchezo wa kuigiza kumhoji Kashilila alikuwa anatoa macho tu kama mbuzi anayekamuliwa maziwa kwa lazima. kwa hiyo lazima awatetee watwana wake CCM. Jamaa pamoja na udaktari wake hajui kuaddress tatizo ambalo linaleta fukuto kubwa la joto. na huyo mtu wa ccm hapo juu ndiyo amesikie leo neno kupotosha? watanzania wenmzake ni akina nani hao anaowasemea? sisi tunaelewa yeye kwa vile kila ktu kikisemwa na ccm ni sawa siyo sisi sote.

    ReplyDelete
  9. Huu ndio mtiririko wa vituko vya wateule wa rais.Na mshahara wake unaidhinishwa na rais,unategemea nini hapo?Siku inakuja tena haiko mbali,watatapika vyote walivyofakamia kwa tamaa na uloho.Huu ndio mtiririko wa vituko vya wateule wa rais.Na mshahara wake unaidhinishwa na rais,unategemea nini hapo?Siku inakuja tena haiko mbali,watatapika vyote walivyofakamia kwa tamaa na uloho.

    ReplyDelete
  10. ha ha ha ha haaaaaaaaa pamoja na umbumbumbu wangu kielimu nadhani kwa hilo la Dk. Kashilila nimempita mbaaaaaaaliiiii sana hana hata IQ ya kumuwezesha kutafakari ipi pumba na upi ni mchele, anajali maslahi ya CCCM inayompa kula kila siku

    ReplyDelete
  11. Kashilila nilimsikia na hoja zake, zaidi sana niliamua kumpuuza maana alichokuwa anaongea ni sawa na kuwafanya watanzania ni watoto wadogo wasioweza kupambanua mambo

    ReplyDelete
  12. jina lenyewe kashilila,msameheni

    ReplyDelete
  13. Mimi nilisoma na huyo Thomas nilishangaa na ninashangaa mpaka sasa aliwezaje kupewa kazi hiyo. Jamani Thomas siadhani kama ana uwezo wa nafasi hiyo ya kazi. Waliompa hiyo kazi ndio wenye makosa. Mimi si CCM wala CHADEMA ila ni mtanzania anayemjua Thomas. Ninawapa pole Watanzania wote kwani mtu kama huyo kupewa nafasi yenye maana katika maisha yao ya kila siku. Huyo bwana hana uwezo wa kuimudu hiyo nafasi.

    ReplyDelete
  14. Huyo Kashilila anajua kuwa anaongea mambo yasiyo kuwa na maana ila anachofanya ni kutetea nafasi yake baati mbaya watu kama yeye ndio walio wengi ndani ya serikali dhaifu ya CCM

    ReplyDelete
  15. Jamani, siku zoote jazba ndio huchukua nafasi ya juu kwenye mambo yote mazito yanayohusu maisha ya Watanzania na unyeti wake. UMEME, UCHUMI, SARAFU, MADINI nk. Sasa hata hili kubwa kabisa la katiba tunalipandishia JAZBA. Labda dakitari Kashilila hana umahiri wa kuvingirisha maneno yakawa na ladha tunayoipenda watanzania, ladha iliyotugeuza kuwa wadanganyika. Huyu Dakitari hajui kuuma maneno, nyeusi ni nyeusi, na sio kijivu au vile:

    Wenzetu wa CHADEMA mmechemsha, ama mmetokosa kabisa. Mmebeba jazba na kwa utaratibu wa kipumbavu na kitoto mkatoka Bungeni bila kusimamia hoja mliokusudia. Hata kama muswada ungepita, pale mgekuwa mmeweka mguu chini na kumlazimisha Spika aite kura kupitisha Muswada. Hii peke yake ingekuwa hatua tosha ya kuwapandisha chati, na Watanzania wangepata fursa ya kusikia hoja zenu, na kwamba kama sio UBABE mbuzi wa CCM na idadi yao kubwa, CHADEMA wana hoja. Lakini mkaingiwa jazba kama kawaida yenu, mkatupa turufu, mkabakiza magarasa!

    Anachowaeleza Kashilila ni TRUTH ya kikatiba na sheria: JK kama Rais, sio mtunga sheria, na hawezi kubadilisha maamuzi ya Bunge. Nachoweza kufanya ni kukataa kuridhia sheria hiyo, jambo ambalo litakuwa ni sawa na kujitwanga nyundo mguuni, kwa faida ya nani?? Na kama aliahidi kutupa Katiba mpya, sasa bila muswada huo atapata wapi fedha na utrataibu mzima wa kukusanya maoni ya wananchi ya Katiba hiyo? Na akipeleka mapendekezo yake kama Rais, halafu Bunge ambalo limesharidhia likiyakataa na kupitisha tena muswada kama ulivyo, je atavunja Bunge ambalo linaongozwa na Chama chake? LABDA kama sasa kaamua kuhamia CHADEMA, jambo ambalo halipo.

    Kashilila kawaambia ukweli wa mambo, CHADEMA wamepeleka zogo kusiko, sioni kwa jinsi gani watalirekebisha tokosa lao la jazba za kiwelaji (aka kivuta bangi/kichomaji)!

    ReplyDelete
  16. Hapana hii Serkali ya kishikaji ndo maana mambo yanaenda muyaonavyo. Kama mnataka kuamini chunguzeni makusanyo yalivyo sasa hawa jamaa wamejipa kila kitu. Matokeo yake W/Fedha imepleka watu wa serkali katika vyuo mbalimbali kwa mantiki kuwa wanawalipia matokeo hadi sasa inaelekea mwezi WA tatu hawajapewa kitu, ila wabunge wao wanaongeza posho na vikao vyao wanalipwa tuu. Sasa hii ni nchi ya namna gani?

    ReplyDelete