Zahoro Mlanzi na Amina Athumani
ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Milovan Cirkovic ametua nchini juzi usiku na muda wowote ndani ya wiki anatarajia
kusaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo.
Kocha huyo atakuwa ni kocha wa tatu katika kipindi cha miaka miwili ndani ya timu hiyo kwani kabla ya kocha wa sasa, Mganda Mosses Basena, alikuwepo Mzambia Patrick Phiri.
Basena inadaiwa kuondolewa katika kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha ufundishaji wake licha ya kwamba ameiacha timu hiyo ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa ikiwa pointi 28.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili ilizipata kutoka vyanzo mbalimbali Dar es Salaam jana, zilieleza kwamba Milovan alitua jijini usiku akitokea kwao Serbia.
“Ni kweli kocha Milovan ametua nchini na jana asubuhi alitakiwa asaini mkataba mbele ya waandishi wa habari lakini kuna vitu inabidi waviweke sawa ndipo amalizane na Simba,” kilisema chanzo hicho bila ya kutotaka jina lake litajwe gazetini.
Kilisema kikubwa kilichokwamisha mpaka jana kocha huyo ashindwe kusaini mkataba ni kwamba kuna vipengele ndani ya mkataba huo bado hawajaafikiana na pia kuhusu suala la mshahara wake.
Walipotafutwa viongozi wa klabu hiyo, Mwenyekiti, Ismail Rage, Makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' kupitia simu zao za kiganjani zaidi ya mara tatu, simu zao ziliita bila kupokelewa.
No comments:
Post a Comment