07 November 2011

Exim yaendesha 'Sajili na Faida Account'

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya Exim Tanzania imeendelea kuimarisha huduma zake ambapo sasa ipo katika kampeni maalumu ya kusajili wateja wapya katika akaunti ya faida ikiwa katika kipindi cha mwezi mmoja imesajili wateja wapya zaidi ya 500.

Meneja Mkuu wa benki hiyo, Dinesh Arora alisema Dar es Salaam hivi karibuni kuwa kampeni hiyo yenye miezi miwili tangu kuanza kwake imelenga kusogeza huduma za benki hiyo karibu zaidi na Watanzania hususani wale wanaofanya shughuli za  kipato cha kati na chini.

Alisema huduma za kibenki kwa jamii ya Kitanzania hususani katika maeneo ya nje ya miji zinaonekana kuwa za watu wenye fedha nyingi kitu ambacho wakati fulani kimekuwa kinawaingizia Watanzania hasara zinazoweza kuepukika.

Arora alifafanua kuwa watu wengi wenye vipato vya kati na chini huweka fedha nyumba kitu ambacho ni  hatari iwapo majanga ya moto na mengine yanayofanana na hayo yatatokea kwa mhusika.

"Ni akaunti inayowalenga watu wa kipato cha kawaida hususani wanaokaa katika maeneo ya nje ya miji ambako huduma za kibenki kwao ni tatizo na wakati fulani kuonekana kama anasa.

"Tunafanya kampeni maalumu kuhakikisha watu hawa wanaingia katika mfumo wa kibenki kwa kujisajili na akaunti yetu ya Faida ili fedha kidogo wanazokusanya kila siku ziwe salama wakati wote," alisema Arora.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa benki hiyo Bi. Linda Chiza alisema tayari timu ya wafanyakazi wao ipo katika maeneo mbalimbali nchini kuhamasisha Watanzania kujiunga na huduma hiyo.
 


'Tukiwekeza katika teknolojia ya mawasiliano uchumi utakuwa'

Na Edmund Mihale 

UCHUMI wa Tanzania utakuwa kati ya asilimia 2 mpaka 3 katika miaka michache ijayo endapo sekta ya Teknolojia ya Mawasiliano na Habari itapewa kipaumbele nchini.

Hayo yalisema na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa wakati alipotembelea Ofisi Kampuni iliyojikita katika Biashara, Teknolojia, njia za kiutatuzi pamoja na Mafunzo ya Techno Brain Tanzania.

Prof Mbarawa alisema Tanzania itafaidika na sekta ya mawasiliano hasa badaya ya kuwekeza kwenye miundombinu (Mkongo wa mawasiliano) na kusema tayari  mikoa 19 imeunganishwa pamoja na wilaya 57 akisisitiza kuwa mkongo huwo itakuwa umefika kilometa 10,000 mwezi wa tatu mwakani.

"Sisi kama serikali tumewekeza katika mradi huu ili kuendeleza eneo hili muhimu katika miundombinu. Mpaka sasa tumeshaunganisha mikoa 19 na wilaya 57. Na ni matumaini yetu kuwa mpaka ifikapo mwezi wa Machi mwaka kesho nchi nzima itakuwa imeunganishwa," alisema.

Alisema kuwa katika kumalizia mradi huwa, kuna umhimu wa kuuanza mchakato wa kufaidisha wananchi wa kawaida na kuhakikisha kuwa watumiaji mbalimbali wa mwisho wafaidika.

"Lugha imeendelea kuwa kikwazo kikubwa katika matumizi ya teknohama. Watanzania  lugha imeendelea kuwa kikwazo kikubwa katika matumizi ya teknohama. Watanzania wengi hawafahamu kingereza. Kama tunaweza kuwa na mfumo wa teknolojia ya habari uliotafsiriwa kwa Kiswahili, itakuwa vizuri. Kampuni kama Techno Brain ikishirikiana na sisi katika hili, ndoto zetu zitafikiwa," alisema.

Awali Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Techno Brain Bw. James Mungai alisema kuwa kampuni yake tayari imefanya kazi mbali mbali na serikali ikiwemo Mfuko wa Hifadhi wa Taifa (NSSF), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)pamoja na kitengo cha Uhamiaji.

 

Meneja Mafunzo wa kampuni hiyo Agnes Munisi alisema kuwa kampuni yake itakuwa imetoa mafunzo kwa wanavyuo 2000 katika vituo vyao sita vilivyopo Afrika ifikapo mwaka 2015.

 

Kampuni ya Techno Brain, ilianzishwa mwaka 1997  na mpaka sasa imejijengea sifa na kuwa miongoni ya Kampini kubwa kwenye sekta ya mawasiliano tayari ikiwa imepata tuzo mbali mbali hapa nchini na





Uuzaji wa hisa EABL waanza kwa kasi

Na Mwandishi wetu


BODI ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Bia ya East African Breweries (EABL) imeridhia uuzaji wa hisa 58,095,693 kwenye Kampuni ya Bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kwa bei ya shilingi 20,60  katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE).

Uuzaji wa hisa hizo ulianza Ijuma ya wiki iliyopita ikiwa ni kutekeleza uuamuzi wa Tume ya Ushindani (FCC) bada ya EABL kununua hisa asilimia 51 kwenye Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na kulazimika kuuza hisa zake za TBL.

Kampuni zitakazo shiriki katika uuzaji wa hisa hizo ni pamoja na Solmon Stockbrokers Limited, National Bank of Commerce (NBC), Orbit Securities Company Limited, Core Securities, Tanzania Securities Limited, Rasilimali Limited, Zan Securities Limited na Vertex International Securities Limited.

Tarifa iliyotolewa na kusainiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TBL Bw. Cleopa Msuya Ijuma iliyopita ilisema kuwa bei ya hisa hizo ni juu kidogo ukilinganisha na bei ambaye hisa za TBL zilikuwa zikiuzwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Orbit ya Orbit Securities Limited ambayo imeteuliwa kuwa mshauri mkuu katika shughuli hizo Laureen Malauri kwenye mahojiano na Majira  alisema wawekezaji walichangamkia kununua hisa hizo siku ya kwanza hisa hizo zilipowekwa sokoni siku ya Ijuma na kuwa na matumaini kwamba hisa hizo zitauzika haraka.

Alisema uuzaji wa hisa za Kampuni hiyo utafungwa Novemba 25 mwaka huu na kuwataka Watanzania kuwa na utamaduni wa kuwekeza kwenye biashara ya hisa.

No comments:

Post a Comment