Na Moses Matthew, Mwanza
KAMATI ya Habari na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilemela Mkoa wa Mwanza, imekamilisha kazi ya kupata maoni mbalimbali kutoka kwa
wananchi ngazi ya Kata kujua sababu zilizosababisha chama hicho kupoteza majimbo mawili ya Ilemela na Nyamagana katika uchaguzi Mkuu uliopita.
Kamati hiyo iliyoanzishwa mwezi Mei na kuanza kazi rasmi mwezi wa saba mwaka jana, imebaini sababu kubwa nne zilizosababisha CCM kushindwa katika majimbo hayo mawili ikiwemo urasimu na ukandamizaji kwa baadhi ya watendaji, walimu kutopewa haki zao kwa wakati, uratatibu wa kura za maoni na migogoro ya ardhi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Jijini hapa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Musa Magabe, alisema lengo kuu la kamati yao kufanya ziara kwenye kata zote za wilaya hiyo ilikuwa kujua kwa undani kero mbalimbali za wananchi wa kada zote wakiwemo wafanyakazi zilizosababisha CCM kunyimwa kura mwaka jana ili ziwasilishwe kwenye kamati ya Siasa ya wilaya na kufanyiwa maamuzi ya utatuzi kwa manufaa ya taifa.
Alisema ili kufikia lengo waligawa kazi hiyo kwa makundi makubwa mawili. Kundi la kwanza ikiwa ni la wananchi na la pili ikijumlisha viongozi wote wa CCM waliokuwa wapigadebe na wasimamizi wakati wa uchaguzi uliopita ili waweze kubaini wapi walipokosea na kujirekebisha mapema.
Akitaja matokeo ya kazi hiyo kwa upande wa wafanyakazi alisema, watumishi wa serikali ngazi za Kata Kamati iligundua udhaifu mkubwa kwa baadhi ya Maofisa wa ngazi ya juu kwenye Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuwanyanyasa walio chini yao hivyo kuwafanya waichukie CCM na serikali yake.
Alitoa mfano kwa watumishi wa sekta ya elimu na kuweka wazi kuwa kamati yake imebaini walimu kukasirishwa na kucheleweshewa mafao yao, malipo yao ya likizo, kupandishwa madaraja na fedha za kujikimu kwa walimu wanaoanza kazi.
Alisema walibaini wananchi wengi wakiwemo wafanyakazi kulalamikia ukiritimba kwa baadhi ya watendaji katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza hivyo kuwafanya waichukie CCM hatimaye kukiadhibu chama hicho kwa kukinyima kura katika uchaguzi mkuu uliopita hususan katika majimbo hayo mawili.
Kwa mujibu wa katibu huyo kero zingine zilizobainishwa na kamati hiyo ni Maofisa watendaji wa kata kutopewa fedha za kuendesha Ofisi na ucheleweshaji wa fedha za maendeleo ikiwemo ukarabati katika sekta za afya, elimu na kero mbalimbali za kijamii.
Kuhusu migogoro ya ardhi alisema kamati hiyo ilibaini wananchi kuchukizwa na kero hiyo kukithiri na kuwapa wakati mugumu katika kata zao na kwamba hawaoni dalili ya wazi kushughulikia tatizo hilo na kwamba waliwekwa wazi kuwa hicho ndicho chanzo cha CCM kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 Jiji la Mwanza.
Akizungumzia viongozi wa CCM ngazi za kata alisema kilio chao kikubwa kilikuwa chama hicho kiliwasahau mabalozi wa nyumba 10 ambao ndiyo uti wa mgongo na uhai wa chama pamoja na mfumo wa utaratibu wa kura za maoni kutosimamiwa vizuri hivyo kuzaa makundi.
Kuhusu suluhisho la matatizo hayo baada ya kazi hiyo Bw. Magabe alisema kuundwa kwa kamati hiyo na kubaini chanzo cha CCM kukosa ushindi wa ubunge na baadhi ya kata ni suluhisho la kwanza kwa kuwa maoni hayo yatawasilishwa sehemu husika na wananchi wataanza kuona mabadiliko.
“Chama cha Mapinduzi hakipindui serikali, kinajipindua chenyewe ndiyo maana unasikia dhana ya kujivua gamba, wananchi watarajie mabadiliko makubwa maana tumeshajua chanzo cha tatizo”, alisema Bw. Magabe.
"Dhana ya kujivua gamba siyo geni, wakati wa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere, alitumia dhana hiyo kwa jina la tujisahihishe katika jitihada za kuweka mambo sawa," alisema.
Hongera bwana Magabe, kama sababu kuu ndio hizo basi bado mtapoteza majimbo hayo labda uenda unazuga tu. CCM needs total overall, the system is completely rotten surviving on police brutality.One day make a survey, visit any popular place where you not known and mention anything praising ccm, I tell you gonna collapse. CCM has nothing new it can offer perhaps to remote areas
ReplyDeleteViongozi wa CCM msiwe wanafiki. Tatizo KUBWA LA KUSHINDWA KWENU NI KUWA HAMTOI FEDHA KWA VIONGOZI WA MASHINA NA WA KATA KANGA, POMBE, SH. 1,000/= HADI 10,OOO/= NA WALI WAMECHOSHWA NAZO. FEDHA ZA KAMPENI HUWA ZINALIWA NA VIONGOZI WAKUU KUANZIA JUU HADI WILAYANI. HAMUONI MAJUMBA, STAREHE, POMBE.GARI ZA KIFAHARI NA HALI NZURI YA MAISHA WALIYO NAYO HAWA VIONGOZI? KWANI MISHAHARA NA MARUPURUPU YAO HAYAFAHAMIKI? FEDHA ZA KAMPENI NI ZA WANA CCM WOTE HATA KAMA ZIMEKUPULIWA SERIKALINI AU KUCHANGWA NA WANACHAMA. YALIYOTAJWA KUSABABISHA KUSHINDWA ILEMELA NA NYAMAGANA NI VISINGIZIO TU! WAPENI WADOGO AMBAO NI WENGI KIKURA PESA ZA KUTOSHA MTASHINDA 2015. NI HAKI YA WADOGO KUPEWA MSHIKO. MMEWAZOESHA.
ReplyDelete