22 November 2011

Kamati Kuu CCM yawaka moto

*Taarifa ya Kamati ya maadili yaumiza kichwa wajumbe

Na Pendo Mtibuche, Dodoma

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. Jakaya Kikwete, amefungua kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho cha siku mbili huku taarifa ya Kamati ya
Maadili ya cama hicho ikiwaumiza kichwa wajumbe kutoa maamuzi mazito.

Kamati ya Maadili ya CCM inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara bw. Pius Msekwa na Katibu wake Bw. Abulrahman Kinana, ilielezwa kuwasilisha taarifa ya kazi yao ya kuwahoji watuhumiwa wanaodaiwa kutaka kukivuruga chama hicho na kutoa mapendekezo mazito ya hatu za kinidhamu kwa baadhi ya viongozi hao.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, baadhi ya vigogo waliotakiwa kuchukuliwa hatu ni wamo pia vigogo wa Umoja wa Vijana wa chama hicho UVCCM, Katibu mmoja wa Mkoa, na wengine.

Ilielezwa kuwa Rais Kikwete alionyesha hali ya ukali tofauti na hali yake ya kawaida huku akiwataka wajumbe 31 waliohudhuria Kikao hicho kutoa mawazo yao kwa uwazi na kwa maslahi ya chama hicjo na si kuangalia mtu.

"Mtihani mzito kwetu ni taarifa ya Kamati ya Maadili, kusema kweli imetuweka njia panda maana ni lazima tutoe maamuzi, mpaka sasa bado mbichi kabisa ila kila kitu kitaeleweka,"kilisema chanzo chetu ndani ya CCM.

Awali akifungua mkutamno huo Rais Kikwete alitumia maneno mafupi ya "kikao kimefunguliwa," kisha kuwaruhusu wajumbe kuanza kazi ya kujadili agenda.

Akitoa taarifa ya utangulizi kwa Rais Kikwete muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao hicho Katibu Mkuu wa CCM Bw. Wilson Mukama, alisema kikao hicho hutakiwa kuwa na wajumbe 38 na kwamba saba wametoa udhuru wa kutohudhuria hivyo kubaki 31.

Awali Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye, akizungumzia dhana ya kujivua gamba ndani ya chama hicho alisema hilo ni sehemu ya mageuzi 26 ndani ya chama chao.

“Ndugu wanahabari nimekuwa nikizungumza na ninyi mara nyingi juu ya mambo mbalimbali ya kukiimarisha chama chetu, niliwahi kuwaeleza kuwa mtu unapotaka kuoga lazima uanzie kichani ndipo ushuke sehemu zingine huwezi kuanza kuoga mwili mzima hivyo hivyo ndani ya chama yapo mambo mengi tuyayoyafanyia kazi si jambo moja tu la kujivua gamaba,”alisema.

Alisisitiza umuhimu wa uadilifu ndani ya chama hicho na kuweka wazi kuwa viongozi wanapaswa kuwa na sifa njema ili waweze kuwatumikia wananchi waliowachagua na kuwaweka madarakani na kwamba mtu akienda kinyume na maadili hatavumiliwa kwa manufaa ya chama na taifa kwa ujumla.

Baada ya Kamati Kuu kumaliza kikao chake leo, kesho ndio kindumbwendumbwe cha Halmashauri Kuu (NEC) kitaanza kikao chake ambacho ndicho kitaridhia maamuzi yote ya Kamati Kuu. Siku ya Ijumaa na Jumamosi kutakuwa na semina maalum kwa watendaji wa chama hicho wakiwemo viongozi wote wa mikoa.

11 comments:

  1. Natamani kutanguliza mkono wa buriani kwa wana mapinduzi hawa kwa sababu sumu waliyonayo haipo kwenye magamba tu, bali imeenea ndani ya damu yao.

    ReplyDelete
  2. There is a party which is preparing its political obituary and many will be dancing on its political grave!
    Tusubiri tuone !

    ReplyDelete
  3. Hili la kuwatimua wasio na maadili "the rotten apples "tuwaachie CHADEMA na ANC ya Afrika kusini kwa CCM ya sasa hili haliwezekani! kwani kuna kiongozi mmoja aliwahi kukiri hadharani kwamba ndani ya chama hicho hakuna aliye msafi!

    ReplyDelete
  4. MW. NYERERE ALISEMA WAZI ITAFIKA WAKATI WATANZANIA WATACHAGUA HATA SHETANI ILIMRADI CCM IONDOKE MADARAKANI KUTOKA NA KUKIUKA MISINGI YA MIZURI YA CHAMA. SASA WATANZANIA WAKO TAYARI KUCHAGUA HILI SHETANI LA KICHAGA ILIMRADI TU CCM IONDOKE. NADHANI CCM ULAFI UMEWAZIDI MAANA HATA HAMJALI TENA KWA CHAMA CHENU KUENDELEA KUSHIKA HATAMU ZAIDI YA KILA MTU KUFIKIRIA MASLAHI BINAFSI.HII NAYO NI LAANA MLIYONAYO.MNAHANGAIKIA MAKUNDI YA URAIS 2015 JE MTAFIKA HUO MKIWA HAI? URAIS NI MGUMU SANA NA WOTE MNAOPAPATIKIA HASA NYIE CCM NA CHADEMA HAMNA DHAMIRA NZURI NA NCHI HII. MLAANIWE

    ReplyDelete
  5. ccm fanyeni kazi mnauzoefu wa kudhibiti wakengeufu. Ukengeufu upo tu kwa kuwa watu mapungufu na jumuiya zao lazima zina mapungufu.kikubwa uzoefu wa kuyadhibiti tuliona azimio la arusha, wahujumu uchumi,fagio la chuma chama tena wakati wa mfumo wa chama kimoja kiliweza kuwadhibiti wakengeufu na sasa wakengeufu kwa jina la mafisadi wadhibitiwe. na anayedhani kuna chama na viongozi malaika anajidanganya binadamu ni KUDHIBITIANA tu full stop.

    ReplyDelete
  6. usilaani usije ukalaaniwa. ninavyoona mimi bora waliopo kikubwa kuwapa presha wasijisahau ila hao wengine wanatisha wanawazoesha watu kutotii wakumbuke wakishika patamu nao wataitwa watawala na kama kawaida waliopo madarakani wataungana na wengine kuwa wapinzani JE! WATAKUWA WAVUMILIVU KAMA JK NA CCM YAKE? au ili kuwatawala watu waliowazoesha maandamano itabidi kuwatisha na hata kuwaua kabisa? tuwe makini

    ReplyDelete
  7. Tusilaumu kabla hatujawapa nafasi. Inawezekana kabisa wakatawala nchi yetu vizuri tena kwa uvumilivu kuliko JK na CCM yake. Utamjuaje mtu na uwezo wake wa kuongoza kabla hujampa nafasi? Wapinzani wapewe nafasi hata kwa kipindi kimoja kama wakishindwa nao tutawaweka pembeni kwa sababu waamuzi ni sisi wapiga kura. Lakini kwa sasa hivi mabadiliko ni lazima ili hata hao CCM wapate muda wa kujirekebisha pamoja na kuwarekebisha hao mafisadi wao vinginevyo kama ni hao hao hatutakaa tupate mabadiliko.

    ReplyDelete
  8. Lowassa ni Baba wa Ubatizo wa uongozi uliopo, aliuweka hawezi kumuengua maana hauna ubavu huo. Wajaribu waone maana hawa akina Nape ni vijana wanaotumiwa kumchafua laikini wamefika mahala wamafeli ajenda zao za siri. Lowasaa ni mchapa kazi na msimamizi mzuri wa mabo ya serikali. Wote tunajua hilo na anaifahamu nchi hii si kiongozi mtalii. Nimemubariki na atakuwa Rais 2015

    ReplyDelete
  9. Nimekubali,una upeo.Mmasai anajua uongozi,ila alichafuliwa ili asije ona uraisi,maana ulikuwa unanukia kwake, lakini kwa kikao cha jana kushnei,atakuwa hana hatia tena,na sijui watamsafishaje hilo neno la ufisadi.itakuwa ni ngumu na atakula nyama ya mtu badala ya ngombe safari hii; list iliyomchafua itajuta kuliona jua,atatumia pesa kuwarudi ndg zangu.urais ndo huo unamnyemelea.raisi mwenyewe kakatisha mjadala jana,amshukuru che-nkapa kumtuliza.

    ReplyDelete
  10. NDUGU Nape asimame auambie umma ukweli kuwa Gamba alilolifakamia ni gumu. alisikika June akisema ukiwa na harufu ya Gongo hata kama hujakutwa unakunywa obvious wewe unasitahili kukamatwa kama mnywa gngo akiwa na maana kuwa hata kama hakuwa na evidence eti akina Lowassa na wenzake ni mafisadi na atawafukuzu Chamani. Sasa Gamba hili limemrudi na litageuka kuwa Rais wa Nchi hii 2015 Nape atajificha wapi. Akomae akatae kutumiwa kisiasa tena wenzake wamemuruka sasa atauaambie jeuri yake i wapi. Hongera Mh Lowassa Mungu akulinde uwe Raisi mwenye hekima na uendelee usimamizi wa kweli kwa mkono wa chuma ili nchi hii uchumi ufufke. Watawala watalii wametuchosha.Usiwaonee aibu wezi wa uchumi ila wasamehe akina NApe na kundi lake.

    ReplyDelete
  11. Ni ajabu lowasa kutamka haya aliyoyatamka baada ya miaka hiyo kupita anafikiri nani atamuamini ktk hili? hata huyo alokuwa m/kiti wa kikao hajui lini na wapi alikuwa kwani safari zake ni nyingi,dunia nzima ilishapewa na kupokea taarifa zake, yeye sasa anataka kubadili upepo uelekee kwa nani?kwa maneno yake anataka uelekee kwa JK na waliokuwa mawaziri na makatibu bado ni CCM tu na ndio maana wameunda kundi la kuitafuna nchi, na hawako tayari kung`atuka na mchezo mnauhamishia ktkt mchakato wa katiba,hatimaye muweke katiba ya kuwalinda mfe mkiwa mmefunikwa bendera ya nchikama mashujaa kumbe uongo.

    ReplyDelete