Na Shufaa Lyimo
UONGOZI wa Klabu ya Azam FC, umesema utahakikisha unakuza na kuinua vipaji vya vijana wenye umri chini ya miaka 20, katika Mikoa ya Kusini.
Akizungumza Dar es Salaam jana na mwandishi wa habari hizo Makamu Mwenyekiti wa Azam, Said Mohamed alisema lengo la kuinua mikoa hiyo ni kupata wachezaji, chipukizi watakaokuja kuwa tegemeo la taifa kwa miaka ijayo.
"Mikoani kuna vipaji vingi, isipokuwa vijana wengi wanashindwa kutoka au kufahamika, kutokana na kukosa wawezeshaji sisi kama Azam, tuna kila sababu ya kuipa kipaumbele mikoa hiyo," alisema Said.
Said alilitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuhakikisha wanapeleka mashindano mbalimbali katika mikoa mingine, kama wanavyofanya Dar es Salaam.
"Viongozi wa TFF, wana kila sababu ya kuisaidia mikoa mingine iweze kupata nafasi ya kufanya mashindano ya vijana, kama wanavyofanya katika Mkoa wa Dar es Salaam," alisema.
No comments:
Post a Comment