24 November 2011

Ajali mbaya yaua wawili Dar

Salim Nyomolelo na Masau Bwire

Wakazi wa Jiji Dar es salaam wakiangalia gari dogo lililoharibiwa vibaya baada ya kugongwa nlori jana
Polisi akiangalia moja ya magari mawili yaliyopata ajali mbaya kwa kugongwa na lori la mafuta T 264 BUC Barabara ya Mandela, Dar es salaam jana.
Askari wa Usalama Barabarani akiwa amebeba Kichwa cha mtu aliyefariki baada ya kugongwa na lori jana maeneo ya Riverside Ubungo Jijini Dar es salaam.
WATU wawili wamekufa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya baada ajali mbaya iliyotokea jana saa saba mchana katika eneo la
Ubungo Riverside, Jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo ilihusisha lori la mafuta lenye namba za usajili T 269 BRQ na tela lenye namba T 264 BUC, ambalo lilikuwa likitoka Ubungo kwenda Buguruni, kuhama upande wa pili wa barabara, kugonga magari saba madogo na kuanguka.

Magari yaliyogongwa ni T 112 BTT aina ya Saloon, T 133 ADC Toyota chesar, T 918 BHC Toyota Colola, T 969 AVM Canter, T 302 AVC Pickup na T 501 BJH aina ya Noah ambayo yalikuwa yakitokea Buguruni kuelekea Ubungo.

Akizungumza na Majira, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, aliwataja waliokufa kuwa ni Bw. Venoni Sebastiani(38) mkazi wa Tabata Kinyelezi, ambaye alikanyagwa na lori hilo wakati akivuka barabara.

Kamanda Kenyela alisema, ajali hiyo pia ilisababisha kifo cha mwanamke mjamzito ambaye jina lake halijafahamika hadi sasa.

“Huyu mwanamke alikuwa akivuka barabara ndipo alipogongwa na lori, kichwa chake kilikatika na kutenganishwa kiwiliwili, rereva wa lori alikuwa akikwepa daladala iliyokuwa ikitoka kituoni wakati akiwa mwendo kasi ndio lihamaha barabara,” alisema.


Aliongeza kuwa, mama huyo alipondwa na kusagika pamoja na kichanga kilichokuwa tumboni.

Aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Bw. Musa Charles (35), mkazi wa Kinondoni ambaye alikatika miguu yote miwili na kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Bw. Yahaya Makame Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wengine ni Bw. Abasi Julius (24), mkazi wa mkazi wa Vingunguti na Bw. Prospa Mwakitaluma (34), mkazi wa Ubungo Changanyikeni ambao wote wamelazwa Hosptitali ya Amana.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, dereva wa gari namba T 302 AVC ambaye alinusurika katika ajali hiyo Bw. Said Sadick, alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa lori ambalo lilikuwa likikwepa daladala.

“Kama angeligonga daladala hilo, angesababisha vifo vya watu wengi zaidi ndio maana alichukua uamuzi wa kulikwepa, daladala husika iliondoka bila kukamatwa,” alisema.

Kwa upande wake, Dereva wa gari namba T501 BJH, ambaye alijitambulisha kwa jina moja Bi. Anna, alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa daladala ambaye alikuwa akitoka kituoni bila kuchukua tahadhari.

7 comments:

  1. Ni msiba mwingine kwa Watanzania. Sijui kama tunajiuliza kama maisha ya watu yana maana yoyote kwetu. Ajali nyingi kwa ni ajili ya uzembe. Ajali zinaleta mahangaiko makubwa kwa wanafamilia wanaobaki! Sijui lini tutajifunza kuchukua tahadhari. Mungu ibariki Tanzania!!!

    ReplyDelete
  2. Madereva wa daladala, wapewe mavunzo rasmi na uendeshaji wa biashara ya daladala uangaliwe ili kuepusha janga hili la ajali kila kukicha

    ReplyDelete
  3. Vifo vingi vya ajali husababishwa na madereva wa magari ya abiria na hili hutokana na kwamba wao wanajua wakati wote wana kipau mbele basi hiyo huwafanya wasitii alama na sheria za barabarani huendesha kwa kuitawala barabara kana kwamba madereva wengine hawana haki na hivyo kusababisha ajali nyingi zaidi USHAURI; jeshi la police kitengo cha usalama barabarani waimarishe alama zote na kuongeza nyingine zinazoonekana na kuweka kamera za kuwanasa madereva wazembe na kuwapa adhabu faini na kuwanyang'anya leseni kwa muda itasaidia

    ReplyDelete
  4. Msiba huu kwa kweli unatisha,na mbaya zaidi hata mzazi nae alikuwemo na kichwa kimetengwa na kiwiliwili chake,mungu walaze pema peponi wasio hatia hawa,Mimi napenda bunge liangalie kwa makini suala hili la usalama wa raia na vyombo vya moto kuanzia majini hadi mabarabarani.
    Kwanza tuangalie thamani ya watembea kandoni mwa barabara kwa sasa hawana dhamani hata ya unywele wao mmoja yaani maisha yao wako chini ya neno mungu yupo.Tuangalie kwa kina nchi zilizofanikiwa kwenye thamani mtu,mfano baadhi ya nchi za asia, ukimgonga mtu na akapata ulemavu wowote basi wewe mwajiri utatakiwa kuikumu familia na yule uliyemgonga katika kipindi chote cha majukumu yake,akifa kama hawa huyo mmiliki wa roli ndiye dhamana ya dereva anatakiwa kuzilipa familia hizo kiasi kisicho pungua 200,000 USD kwa kila familia,iwe kufirisi au kuzuia mali,na huyo dereva wa daladala ni miaka 7 jela bila dhamana.
    Basi kwa hilo mimi ombi langu tuweke mazingira ya wenye magari kuwaogopa watembea kwa miguu kutokana thamani waliyonayo na hii pia itasaidia hata mabasi ya mikoani kupunguza ajali kwani kama uzembe utatokea basi familia za wahusika ni kwamba zipo chini yao.

    Mungu tubaliki wanyonge wamulikwe,

    ReplyDelete
  5. Madereva wa daladala hazingatii sheria. Mimi nashauri viongozi waige mfano kwa mheshimiwa Rais Kagame. Madereva wanatakiwa wawe wanachapwa viboko hadharani na faini hapo tatizo la kuchomekea litaisha.

    ReplyDelete
  6. jamani ajali inatisha kweli kama hiyo ya mwanamke kusagika na kachanga tumboni kichwa kugawanyika ooooooooooohhhhhhhhh my lord. Inauma hadi kizunguzungu. jamani ninyi madereva daladala mmezidi sasa na sisi wananchi bila daladala huendi popote jamani muwe makini inaniuma sana.

    ReplyDelete
  7. Ni kweli madereva hasa wa daladala wamekuwa kama vichaa serkali iongeze adhabu ya kuchapwa viboko tena hadharani mimi nadhani itatusaidia ingawa kidogo kupunguza dhahama hii

    ReplyDelete