Na Rachel Balama
SERIKALI imetakiwa kusitisha ombi la dharura la kupandisha bei ya umeme kwa kiwango kikubwa ili kuepusha athari katika usalama na
uchumi kutokana na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha.
Pia serikali imetakiwa kuchukua hatua za haraka kulinusuru Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) dhidi ya mzigo mkubwa wa gharama unaotokana na ufisadi wa muda mrefu katika mikataba ya gesi asilia na gharama za mitambo ya kufua umeme wa dharura badala ya kuweka mkazo katika kuongeza bei ya umeme kwa wananchi wa kawaida.
Taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es salaam jana na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia CHADEMA, Bw. John Mnyika.
Alisema kuwa izingatiwe kuwa Novemba 9, mwaka huu Mamlamka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea ombi la dharura toka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kuidhinisha ongezeko la bei za huduma ya umeme kwa wastani wa asilimia 155 ya bei ya sasa (zaidi ya mara tatu).
Bw. Mnyika amewaomba wananchi kushiriki kwa wingi katika mkutano wa kukusanya maoni ya wadau ulioitishwa na EWURA ifikapo Desemba 2, mwaka huu.
Aliutaka Umma wa watanzania ufahamu kwamba ongezeko hilo sio ombi la TANESCO pekee bali ni agizo kutoka kwa serikali kwa kurejea maelezo ya Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja katika kikao cha bunge kilichopita.
Alisema hii ni mara ya pili katika kipindi cha takribani mwaka mmoja kwa TANESCO kupandisha bei ya umeme ambapo kwa mara ya kwanza ilikuwa ni mwezi Januari mwaka huu ambapo umeme ulipanda kwa asilimia 18.5 na kuchangia katika kupanda kwa gharama za uzalishaji katika nchi na kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.
Alisema ombi la TANESCO la wakati huo la kupandisha umeme lilikuwa ni asilimia 34 likakataliwa na EWURA na kushushwa mpaka asilimia 18.5, sasa Rais Kikwete, Waziri Mkuu Pinda na Waziri Ngeleja wanapaswa kuwaeleza watanzania sababu za kufanya ombi hilo la dharura kuwa la wastani wa asilimia 155 ili wananchi waweze kutoa maoni kwa kuzingatia mzigo ambao umma unataka kubebeshwa.
Pamoja na matatizo ya kifedha ya TANESCO ambayo serikali inapaswa kuyashughulikia kwa pamoja na mambo mengine kutoa ruzuku katika kipindi hiki cha mpito.
Alisema gharama kubwa za uzalishaji zinazolikabili shirika zinachangiwa na ufisadi wa muda mrefu katika mikataba ikiwemo ya uzalishaji wa gesi na ukodishaji wa mitambo ya kufua na pia maamuzi ya kukopa kibiashara katika kutekeleza mpango wa dharura wa umeme.
Aliongeza kuwa Kabla ya kuongeza bei ya umeme kwa watanzania wa kawaida, Serikali ieleze imewapunguzia mzigo kiasi gani wananchi kwa kupitia upya mikataba ya kifisadi inayolinyonya Shirika la Umeme Tanzania.
Alisema uamuzi wa kupandishwa kwa kiwango kikubwa bei ya umeme utasababisha ongezeko la ziada la mfumuko wa bei hali ambayo ni tishio wa usalama na uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla.
Alisema serikali izingatie kwamba mfumuko wa bei nchini hivi sasa umefikia asilimia 17.9 na bidhaa zinazochangia mfumuko huo kwa kiwango kikubwa ni vyakula, mafuta na umeme.
Alisema kauli iliyotolewa na rais katika hotuba yake kwamba mfumuko wa bei na kuporomoka kwa thamani ya shilingi nchini dhidi ya dola kumetokana na uchumi wa nchi mbalimbali duniani hususani za Ukanda wa Sarafu ya Ulaya kuwa katika kipindi kigumu na cha mashaka na kueleza kwamba suluhisho la tatizo la uchumi wetu litategemea uchumi wao.
Alisema kauli hiyo imedhihirisha kwamba Serikali haina mpango wa haraka wa kukabiliana na mfumuko wa bei, kuporomoka kwa shilingi na kupanda kwa gharama za maisha.
Alisema mpango wa kupandisha bei ya umeme kwa wastani wa asilimia 155 unapaswa kusitishwa au kubadilishwa kwa kulinda maslahi ya makundi mbalimbali kwa kuzingatia aina za matumizi.
Hii inaweza kuchafua hali ya amani, jamani hawa viongozi wako wapi?
ReplyDeletewakati umefika wa kuchafua amani ya nchi. ongezeko la 10-15% lingeeleweka lakini kiwango wanachotaka kinaleta kizunguzungu. tunajua wanatafuta hela ya kuwalipa dowans lakini wasiwachukue walalahoi rehani kulipia madhambi yao ya 10%. si akina lowassa, karamagi na msabaha bado wako hai na wanapeta na utajiri wa mkato wao kwenye mikataba mibovu? basi walipe!
ReplyDeleteWe are tired of been given the budden of carrying the nation debts,I remember last year all the Tanesco employees were given an insurance of Twenty million each,The contract was suddenly terminated this year 2011 may,How come this contract came up only in the year of elections after a year later the contract has been terminated ,THis was just a way of stealing the money by CCM to fund there campaigns,Now this time they are putting the budden on its citizens pliz CCM have mercy on us
ReplyDeleteOmbi la nyongeza kwa asilimia yoyote kwa sasa halikubaliki. Hii ni kumlazimisha mlala hoi kuzidi kutunisha mifuko ya mafisadi ambao tayari wana mabilioni kama si matrilioni kwenye akiba zao. Kama hali ni hiyo iliyotekea hivi karibuni kwa TANESCO kati ya idara nyingine kuchanga milioni hamsini ambazo zinaingia kufukoni na kuacha mwenye kipato chini ya Tsh. 1000 akilia kwa kushindwa kununua unit 4.20 za umeme, je, ukipandisha zaidi maana yake nini? Tusiwasababishe wanachi wa hali ya chini kuichoka serikali yao.
ReplyDelete