Grace Ndossa na Rachel Balama
BAADHI ya wananchi wakiwemo wanasiasa wametoa maoni yao kuhusu muswada wa mabadiliko ya katiba uliotangazwa na
serikali katika vyombo vya habari jana na kuhoji uhalali wa rais kuachiwa nguvu kubwa zaidi na madaraka ya kuteua wajumbe wa tume itakayoratibu mchakato mzima.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jana, wananchi hao walisema wamekerwa na kitendo cha rais kupeGrace Ndossa na Rachel Balama
BAADHI ya wananchi wakiwemo wanasiasa wametoa maoni yao kuhusu muswada wa mabadiliko ya katiba uliotangazwa na serikali katika vyombo vya habari jana na kuhoji uhalali wa rais kuachiwa nguvu kubwa zaidi na madaraka ya kuteua wajumbe wa tume itakayoratibu mchakato mzima.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jana, wananchi hao walisema wamekerwa na kitendo cha rais kupewa madaraka makubwa juu ya uundwaji wa tume pasipo kuwashirikisha wananchi.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUTI) Profesa Mwesiga Baregu ambaye pia ni mwanasiasa mshauri wa CHADEMA alisema serikali imekosa usikivu na umakini kwa wananchi kutokana na kipengele kinachompa rais madaraka.
Alisema muswada kwa mara ya kwanza ulikataliwa bungeni na kurudishwa kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho lakini bado anashangaa kuona kipengele hicho kimerudiwa tena.
"Sehemu ya tatu juu ya uundaji wa tume kipengele cha tano kinasema Rais baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar na kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na kwa kuzingatia hali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi iliyopo katika Jamhuri ya Muungano katika nyakati zote na kwa amri iliyochapishwa katika gazeti la serikali, ataunda tume,"alisema Prof.Baregu
Alisema kipengele hicho hakikustahili kuwepo kwa kuwa katiba inayoundwa ni katiba ya hatma ya maisha ya watanzania na kuhoji uhalali wa mtu mmoja kupewa jukumu hilo.
Alisema kwa mtazamo wake uenda muswada huo ukarudishwa tena kwa ajili ya marekebisho kutokana na kipenge hicho kilitakiwa kuondolewa.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) Bw.Hassan Kisabya, alisema upo umuhimu wa kurekebisha baadhi ya vipengele na kuwashirikisha wananchi.
"Ni vyema wakaangalia tume itakayoundwa kuwashirikisha watu wa aina mbalimbali ili mwisho wa siku haki iweze kutendeka," alisema.
Hata hivyo alisema upo umuhimu wa mambo kuendeleza mambo mazuri yaliyopo kwenye katiba ya sasa kuingizwa moja kwa moja kwenye katiba mpya kwa manufaa ya taifa.wa madaraka makubwa juu ya uundwaji wa tume pasipo kuwashirikisha wananchi.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUTI) Profesa Mwesiga Baregu ambaye pia ni mwanasiasa mshauri wa CHADEMA alisema serikali imekosa usikivu na umakini kwa wananchi kutokana na kipengele kinachompa rais madaraka.
Alisema muswada kwa mara ya kwanza ulikataliwa bungeni na kurudishwa kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho lakini bado anashangaa kuona kipengele hicho kimerudiwa tena.
"Sehemu ya tatu juu ya uundaji wa tume kipengele cha tano kinasema Rais baada ya kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar na kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na kwa kuzingatia hali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi iliyopo katika Jamhuri ya Muungano katika nyakati zote na kwa amri iliyochapishwa katika gazeti la serikali, ataunda tume,"alisema Prof.Baregu
Alisema kipengele hicho hakikustahili kuwepo kwa kuwa katiba inayoundwa ni katiba ya hatma ya maisha ya watanzania na kuhoji uhalali wa mtu mmoja kupewa jukumu hilo.
Alisema kwa mtazamo wake uenda muswada huo ukarudishwa tena kwa ajili ya marekebisho kutokana na kipenge hicho kilitakiwa kuondolewa.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA) Bw.Hassan Kisabya, alisema upo umuhimu wa kurekebisha baadhi ya vipengele na kuwashirikisha wananchi.
"Ni vyema wakaangalia tume itakayoundwa kuwashirikisha watu wa aina mbalimbali ili mwisho wa siku haki iweze kutendeka," alisema.
Hata hivyo alisema upo umuhimu wa mambo kuendeleza mambo mazuri yaliyopo kwenye katiba ya sasa kuingizwa moja kwa moja kwenye katiba mpya kwa manufaa ya taifa.
huyo mwesiga yeye ni kama nani? asitake kutuletea siasa kwenye katiba, yamemshida UDSM sasa anataka kuwaharibia hata hao wa madhehebu ya dini(SAUT)kwakweli huyu jamaa siku zote yeye ni mtu wa kuharibu, anasiasa za chuki wakati UDSM palimshinda akaondoka kwa uchu wa kutaka siasa sasa anataka kutuambia nini kwani yeye pia yupo kwenye Mchakato wa kutaka nchi isitawalike. hilo tunalijua na washirika wake wote tunawajua.Watanzania wenye nia thabiti na nchi hii tunawajua na pia wababaishaji kama kina mwesiga tunawajua. Ukweli Chadema sasa wameanza kupoteza Dira na bado ile picha ya maovu yao itaonekana vizuri ukikaribia Uchaguzi wa 2015. Watanzani tunataka Amani na Utulivu katika kuelekea kupata Katiba Mpya. Kwa kuwa iliyopo inayo mazuri yake.
ReplyDeleteraisi ni mwajiriwa wa wananchi iweje sasa awapangie cha kufanya matajiri wake? maajabu ya mungu mbona mnakotupeleka siko?
ReplyDelete