Na Zahoro Mlanzi
TIMU ya taifa ya wanawake (Twiga Stars), imepangwa kucheza na Namibia katika mechi ya mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za nane za Kombe la Mataifa ya
Afrika kwa Wanawake.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema mechi ya kwanza itachezwa jijini Windhoek, Namibia kati ya Januari 13, 14 na 15, mwakani na marudiano itachezwa Dar es Salaam kati ya Januari 27, 28 na 29 mwakani.
Alisema iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Namibia, katika raundi ya kwanza itacheza na mshindi wa mechi kati ya Ethiopia na Misri, ambazo pia zinaanzia raundi ya awali.
"Mechi ya awali ya raundi ya kwanza, itachezwa ugenini kati ya Mei 25, 26 na 27 mwakani na mechi ya marudiano itachezwa kati ya Juni 15, 16 na 17 mwakani," alisema Wambura.
Alisema timu ambazo zinaanzia moja kwa moja raundi ya kwanza kutokana na kuwa juu katika viwango vya ubora ni Afrika Kusini, Cameroon, Guinea ya Ikweta na Nigeria.
Twiga Stars hivi karibuni ilishiriki mashindano ya Afrika (All African Games) iliyofanyika jijini Maputo, Burundi lakini haikufanya vizuri.
No comments:
Post a Comment