07 October 2011

Mnigeria kuwasindikiza BSS

Na Amina Athumani

MSANII wa muziki kutoka nchini Nigeria,  N’Abania 'Mr Flavour',  amealikwa kutumbuiza katika fainali za mashindano ya kuibua vipaji ya Bongo Star Search  Second Chance,  itakalofanyika
Oktoba 14, mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Msanii huyo anayetamba na kibao chake cha Ashawoo katika vituo mbalimbali vya redio nchini, atafanya onesho hilo pamoja na wasanii wengine nchini.

Akizungumza Dar es Salaam jana,  Mkurugenzi wa Benchmark Production ambao ndio waratibu wa shindano hilo, Ritha Paulsen, alisema msaniii huyo atatua nchini Oktoba 12 akitokea nchini Nigeria.

Ritha  alisema kuwa, washiriki katika fainali hiyo, washiriki wanne watashindana, ambapo mshindi ataondoka na kitita cha sh. milioni 40.

MKurugenzi huyo alisema mshindi wa pili atazawadiwa sh. milioni 10 na mshindi wa tatu sh. milioni 5.

Alisema tiketi za onesho hilo zitaanzwa kuuzwa Oktoba  11,  katika vituo vya Shear Illusion, Beauty Pointi, Big Respect, Manywele Entertainment na Diamond Jubilee.

 Washiriki  watakaopanda jukwaani kushindana na namba zao za kuwapigia kura ni Waziri Salum (BSS 23), Rogers Lucas (BSS  27), Bella Kombo (BSS 05) na Haji Ramadhani (BSS  11).

No comments:

Post a Comment