LONDON, Uingereza
ARSENE Wenger amesema kuwa, kati ya timu za England zilizopo kwenye Ligi ya Mabingwa, hakuna inayoweza kufanana na Barcelona au Real Madrid.Kwa
mujibu wa gazeti la Mirror, kocha huyo wa Arsenal, ambaye timu yake ilicheza dhidi ya Dortmund katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Kundi F, alisema: "Timu mbili zilizo juu ya zote, Real Madrid na Barcelona.
"Nyingine zitajipanga wakati wa msimu. Ushindani wa ndani kwenye nchi yetu umekuwa mkubwa. Na nje, Barcelona na Real Madrid wana nguvu ya fedha.
"Kwetu, ni mwanzo mpya kwa kuwa, tuna kikosi kipya.
Alisema kuwa, timu yake katika ligi ya mabingwa itacheza kwa uwezo wake wote ili iwe kusonga mbele.
Alisema Real na Barcelona, zimeonesha uwezo mkubwa na kwamba, wanaweza kutwaa kitu, ni mapema sana kuwalinganisha na wao.
"Ni mapema sana kulinganisha uchezaji wa Manchester City na wa Barca.
Alisema hasemi hivyo kwa kutowapa sifa Man City, lakini wachezaji wa Barca wametwaa ubingwa wa Dunia na timu imetwaa ubingwa wa Ulaya mara mbili katika misimu mitatu, kitu ambacho anaona kuwa ni mapema kuifananisha na City."
No comments:
Post a Comment