*CUF yawawekea pingamizi, yadai hawana sifa
*Mkurugenzi wa uchaguzi ataka vielelezo vyao
Na Peter Mwenda, Igunga
Alisema kuwa mgombea wa CHADEMA Bw. Kashindye ni mfanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akiwa na
wadhifa wa Mkaguzi wa Elimu Wilaya ya Igunga, wakati mgombea wa CCM Dkt. Kafumu ni Kamishina wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Igumga Bw. Protace Magayane, alisema kuwa amepokea pingamizi hilo na anatoa nafasi kwa walalamikiwa kutoa vielelezo kabla hatua hazijachukuliwa.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Vijana Taifa wa CUF Bw. Mohamed Babu amekanusha tuhuma zilizoelekezwa kwao kuwa wao ni chanzo cha vurugu zilizosababisha mtafaruku wakati wa kurudisha fomu za wagombea wa Chama hicho na CHADEMA.
Alisema kuwa wafuasi wa CHADEMA ndio walikuwa wa kwanza kumzuia mgombea wa CUF Bw. Leopoad Mahona asiweze kurudisha fomu katika kipindi hicho ambacho na wao walikuwa wamejiandaa kurudisha fomu za mgombea wao.
Hata hivyo Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Igunga Bw. Christopher Saye alisema nao wamewasilisha malalamiko yao kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo (OCD) wakidai kuwa walifanyiwa fujo.
No comments:
Post a Comment