20 September 2011

Timbe awatupia lawama wachezaji

Na Mwali Ibrahim

KOCHA Mkuu wa Yanga Sam Timbe, amewatupia lawama washambuliaji wake kwa kupata nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kuzitumia katika ya mechi ya Ligi Kuu Bara
dhidi ya Azam FC iliyochezwa Juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Timbe alisema katika mechi hiyo, ambayo walifungwa bao 1-0, washambuliaji hao walionesha udhaifu wa kufunga mabao licha ya kupata nafasi nyingi za wazi.

Alisema kushindwa kuzitumia nafasi hizo, kuliwafanya mabeki kufanya kazi ya ziada ya kupanda mbele kusaidia kitu kilichowachosha.

Timbe alisema baada ya kuona makosa hayo, atalazimika kuyafanyia kazi ili yasijuridie katika mechi nyingine za ligi hiyo.

Alisema amesha kubali matokeo waliyoyapata katika mechi hiyo kwa kuwa katika mashindano kuna kufungwa na kufunga.

Kocha huyo amewataka wana-Yanga, kuondoa hofu kwa timu yao kwani makosa yanayoonekana sasa ni madogo na tayari wanajipanga upya.

No comments:

Post a Comment